UN: Hali ya kibinadamu huko Goma bado ni mbaya licha ya kusimamishwa mapigano

Hospitali katika mji mkubwa wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Goma, zinatatizika kutibu mamia ya wagonjwa waliojeruhiwa, huku baadhi wakiripoti uhaba wa dawa siku chache baada ya kundi la waasi la M23 kutangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja.