UN: Hali ya Goma DRC imetulia, kuna ufyatuaji risasi na uporaji wa hapa na pale

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba, hali katika mji wa Goma wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ni shwari lakini bado ni ya wasiwasi, huku baadhi ya vurugu zikikwamisha shughuli za kibinadamu.