
Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa, wanawake na watoto wanaunda asilimia kubwa ya vifo na majeruhi wa mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imesema katika ripoti yake mpya kuwa, asilimia 70 ya Wapalestina waliouawa au kujeruhiwa katika mzozo wa Gaza ni wanawake na watoto wadogo.
Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Elnashra, huku utawala wa Kizayuni ukiendeleza hujuma za kinyanama Gaza, makundi ya Muqawawama ya Wapalestina nayo yanaendelea na operesheni zao za kijeshi dhidi ya vikosi vamizi na zana za kivita huko Gaza.
Vita vilivyoanzishwa na utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza vimezusha mzozo wa kibinadamu ambao haujawahi kushuhudiwa, na kusababisha zaidi ya asilimia 85 ya wakazi wa eneo hilo (sawa na takriban watu milioni 1.9) kuwa wakimbizi.
Tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari vya utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Gaza Oktoba mwaka jana, zaidi ya Wapalestina 43,400 wameuawa shahidi na zaidi ya 102,500 kujeruhiwa, akthari yao wakiwa ni wanawake na watoto.