Umoja wa Mataifa yaonya kuhusu Israel kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, utawala wa Kizayuni unazuia misaada ya kibinadamu kuingia katika Ukanda wa Gaza.

Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk amebainisha hali ngumu na mbaya inayowakabili watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa kwamba, ni jambo lisilowezekana kuishi katika Ukanda wa Gaza.

Aifa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, ikiwa vita havitakoma vitakuwa kama virusiii kkwanii vitaenea katika maeneo mengine.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa sambamba na kuashiria kuwa zaidi ya Wapalestina 42,000 wameuawa shahidi katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, ametoa wito wa kuingilia kati mashirika ya kimataifa na nchi za dunia ili kukomesha machungu na mateso makubwa wanayokumbana nayo Wapalestina katika hususan katika Ukanda wa Gaza.

Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa

Kwa mwaka moja sasa jeshi katili la Israel linasonga mbele na mashambulizi yake ya mara kwa mara katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa sasa zaidi ya mwaka mmoja katika vita vya mauaji ya kimbari.

Mashambulizi ya utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Gaza yalianza Oktoba mwaka jana, na hadi sasa utawala huo umeua karibu Wapalestina 43,000. Zaidi ya wengine 98,000 pia wamejeruhiwa tangu wakati huo.