Umoja wa Mataifa wataka kusitishwa mapigano katika Ukanda wa Gaza na Lebanon

Umoja wa Mataifa umesisitizia wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon na katika Ukanda wa Gaza kama njia moja ya kuzuia kutokea kwa mzozo zaidi mashariki ya kati, hatua ambayo UN inasema itaadhiri dunia nzima.

Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa shirika la wakimbizi UNHCR unaofanyika mjini Geneva, Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi ameeleza kwamba, mapigano yanatakiwa kusitishwa mara moja.

Wito wake umekuja wakati huu utawala wa Kizayuni wa Israel ikiripotiwa kuendelea kutekeleza mashambulio inayosema yanawalenga wapiganaji wa Hezbollah.

Wakati hayo yakijiri jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeishambulia kwa mabomu kambi ya wakimbizi katika eneo la kati la Ukanda wa Gaza na kusababisha moto mkubwa uliopelekea kuuawa shahidi Wapalestina waliokuwa wametafuta hifadhi kwenye eneo hilo kutokana na hilaki ya vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala huo ghasibu.

Jinsi Gaza ilivyoharibiwa kwa mashambulio ya anga ya jeshi la utawala haramu wa Israel

Mashambulizi hayo yaliyofanywa jana, yalilenga kambi iliyowahifadhi Wapalestina waliolazimika kuyahama makazi yao na kukimbilia kwenye uwanja wa Hospitali ya Mashahidi wa al-Aqsa katika mji wa Deir al-Balah, na kuua watu wasiopungua wanne na kujeruhi wengine wapatao 70.

Katika uchunguzi wake, Human Rights Watch pia ilithibitisha kutumiwa mabomu hayo na jeshi la Israel katika manispaa zisizopungua 17 kusini mwa Lebanon tangu Oktoba 2023, wakati lilipoanzisha vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Tangu vilipoanza vita hivyo, Marekani imekuwa ikiisaidia Israel kikamilifu katika masuala ya silaha na mabomu.