Umoja wa Afrika umeondoa vikwazo dhidi ya Gabon na kuirejesha katika taasisi zake

Gabon yajiunga tena na Umoja wa Afrika. Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC) ambalo limekutana leo Jumatano asubuhi, Aprili 30, mjini Addis Ababa, limeamua kuondoa vikwazo dhidi ya Libreville hususa kusitishwa kwake katika taasisi za baraza hilo, miezi 20 baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Agosti 2023.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Amani na Usalama la AU, ambalo limeona kuwa mpito uliopindua Ali Bongo “umefanikiwa kwa ujumla,” kwa hivyo limeamua kuondoa mara moja vikwazo vilivyowekwa kwa Gabon,” kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, ikizingatiwa kuwa mchakato wa kisiasa wa Gabon “ni wa kuridhisha.” 

Uamuzi huu unakuja siku tatu kabla ya kuapishwa kwa Brice Clotaire Oligui Nguema, aliyechaguliwa kuwa rais wa nchi mnamo Aprili 12.

Gabon, kama nchi nyingine ambazo zimekumbwa na mapinduzi ya kijeshi katika miaka ya hivi karibuni, kama vile Mali, Burkina Faso, na Guinea, ilikuwa imesimamishwa na Umoja wa Afrika na haikuweza kushiriki katika uchaguzi wa mwezi Februari wa rais mpya wa Tume yake.

Gabon ilitawaliwa kwa mkono wa chuma na familia ya Bongo kwa zaidi ya miongo mitano, kwanza na Omar Bongo kuanzia mwaka 1967 hadi mwaka 2009, kisha mwanawe Ali ambaye alimrithi hadi alipopinduliwa mwaka 2023 na Brice Clotaire Oligui Nguema.

Jenerali huyo, baada ya kipindi cha mpito, alichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo ndogo ya Afrika, yenye wakazi wachache lakini yenye utajiri wa mafuta, mwezi Aprili, kwa asilimia 94.85 ya kura.

Kwa mujibu wa katiba mpya, rais aliyechaguliwa ataichukua nchi akiwa na mamlaka yaliyoongezwa. Nafasi ya Waziri Mkuu ilifutwa kwa ajili ya kuundwa kwa wadhifa wa makamu wa rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *