
Ukraine imetangaza siku ya Jumapili kwamba mabadilishano na Urusi ya wafungwa na miili ya wanajeshi waliouawa, yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili, yatafanyika “wiki ijayo,” baada ya Moscow na Kyiv kulaumiana kwa kuchelewesha mchakato huo.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Kuanza kwa shughuli za kuwarejesha makwao, kwa kuzingatia matokeo ya mazungumzo ya Istanbul, imepangwa wiki ijayo (…) Kila kitu kinakwenda kama ilivyopanwa,” amesema mkuu wa idara ya wa kijeshi wa Ukraine, Kyrylo Budanov, akiishutumu Moscow kwa “mchezo usio wa haki.”
Siku ya Jumamosi, kiongozi wa ujmbe wa Urusi katika mazungumzo huko Istanbul, Vladimir Medinsky, alisema kwamba “upande wa Ukraine umeahirisha bila kutarajia upokeaji wa miili” ya askari waliouawa “na kubadilishana kwa wafungwa wa vita hadi tarehe ambayo haijatajwa.” Mabadilishano haya, yaliyopangwa wikendi hii kulingana na Moscow na Kyiv, yalikuwa matokeo madhubuti ya mazungumzo ya moja kwa moja ya Urusi na Ukraine nchini Uturuki siku ya Jumatatu.
Pande hizo mbili zilikubali kuwaachilia wafungwa wote wa vita waliojeruhiwa vibaya au wagonjwa, pamoja na wale walio na umri wa chini ya miaka 25, jambo ambalo lingefanya mabadilishano haya kuwa makubwa zaidi ya vita baada ya ya ya awali yaliyohusisha watu 1,000 kila upande mwezi Mei. Kufuatia mazungumzo ya Istanbul, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alihakikisha kwamba yatafanyika mwishoni mwa juma hili, na Urusi ilisema iko tayari kwa Jumamosi, Jumapili au Jumatatu.
Mashambulizi katika mkoa wa Dnipropetrovsk
Siku ya Jumamosi, Moscow ilidai kupeleka orodha kwa Ukraine ambayo ilisema “haikuendana” na masharti ya makubaliano. Kuhusu mabaki, mpatanishi wa Urusi Medinsky alitoa wito kwa Kyiv “kuokoa miili ya wanajeshi 6,000 wa Ukraine,” ambao “1,212 tayari wako kwenye eneo la kubadilishana wafungwa.” Ukraine ilijibu kwamba “hakuna tarehe amayo imetangazwa.”
Shutuma hizi zinakuja baada ya mashambulizi makubwa ya usiku ya Urusi dhidi ya Ukraine, kufuatia ahadi ya Moscow ya “jibu” kwa uharibifu wa sehemu ya meli zake za kivita siku ya Jumapili iliyopita. Mashambulizi haya yaliendelea hadi siku ya Jumamosi, na kusababisha jumla ya watu kumi kuuawa katika ardhi ya Ukraine. Katika Kharkiv, mji wa pili kwa ukubwa wa Ukraine na uliolengwa mahususi, watu wanne waliuawa na angalau 22 kujeruhiwa, kulingana na mamlaka ya kikanda.
Siku ya Jumapili, jeshi la Urusi limetangaza kufanya mashambulizi katika eneo la Ukraine la Dnipropetrovsk, linalopakana na eneo la Donetsk, tukio ambalo ni la kwanza katika zaidi ya miaka mitatu ya mzozo. Kuingia kwa jeshi la Urusi katika eneo la Dnipropetrovsk (kati-mashariki mwa Ukraine), ambalo halijathibitishwa na Ukraine, kungeashiria kurudi nyuma kwa ishara kwa vikosi vya Ukraine, vinavyopambana kwenye mstari wa mbele kwa sababu ya ukosefu wa askari na silaha za kivita.
Siku ya Jumapili jioni, Zelensky aliikashifu tena Urusi: “Upande wa Urusi, kama kawaida, unajaribu kucheza mchezo mchafu na wa kisiasa,” alisema katika hotuba yake ya jioni, na kuongeza kwamba ikiwa Moscow haitaheshimu makubaliano hayo, “itatilia shaka sana” juhudi za kidiplomasia zinazolenga kumaliza vita ambavyo vimedumu kwa zaidi ya miaka mitatu.