Ukraine yaanza mazungumzo muhimu na Marekani nchini Saudi Arabia

Ni kwenye ufuo wa Bahari Nyekundu huko Jeddah, Saudi Arabia, ambapo mkutano muhimu unafanyika Jumanne, Machi 11, kati ya wawakilishi wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na wale wa Rais wa Marekani Donald Trump. Mkutano huo unakusudiwa kutafuta njia za kumaliza vita nchini Ukraine, lakini hasa utakuwa juu ya kurejesha uhusiano kati ya Kyiv na Washington, kufuatia purukushani kati ya viongozi wa nchi hizo mbili katika Ikulu ya White House mnamo Februari 28.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

“Mkutano kati ya wajumbe wa Ukraine na Marekani unaanza Jeddah, Saudi Arabia,” wanadiplomasia wa Ukraine wameandika kwenye Telegram leo Jumanne, Machi 11, wakirusha video fupi ambayo maafisa wa Ukraine wanaweza kuonekana wakiingia kwenye chumba cha mazungumzo. Itakuwa mara ya kwanza tangu mzozo wa Oval Office ambapo wawakilishi kutoka nchi hizo mbili kukutana rasmi. Kwa upande wa Ukraine, kutakuwa na Andrii Yermak, mkuu wa utawala wa rais, na mawaziri wa ulinzi na mambo ya nje. Kwa upande wa Marekani, Marco Rubio, mkuu wa diplomasia ya Marekani, na mshauri wa usalama wa taifa Mike Waltz watakuwepo.

Pendekezo la kusitisha mapigano angani na baharini

Kulingana na shirika la habari la AFP, ujumbe wa Ukraine utaleta pendekezo la usiishaji mlapigano na Urusi angani na baharini, chaguo la kusitisha mapigano ambalo ni rahisi kutekeleza na kufuatilia. Kyiv inatumai kuishawishi Marekani kurejelea uamuzi wake wa kusitishwa kwa msaada yake wa kijeshi.

Ishara ya kutia moyo ilionekana katika mkesha wa mkutano: Marco Rubio alisema alikuwa na matumaini ya kusonga mbele katika suala hili. Lakini zaidi ya matokeo madhubuti yanayoweza kutokea ya mkutano huo, changamoto itakuwa ni kufuta kumbukumbu mbaya ya Februari 28 na kurekebisha uhusiano ulioharibiwa sana kati ya Ukraine na mshirika wake mkuu.

Wakati huo katika mabadilishano makali katika Ofisi ya Oval, Rais wa Marekani Donald Trump alimuonya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwamba “anacheza kamari na maisha ya mamilioni” na kuzidisha hatari ya “Vita vya Tatu vya Dunia.”

Trump alisisitiza kwamba Zelenskyy lazima afanye makubaliano au akabiliane na matokeo mabaya, akisema, “Tutafikia makubaliano, au tuachane nayo na wewe uendelee na hili suala peke yako.”

Akiwa ndani ya ndege kuelekea Saudi Arabia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alionya kwamba Marekani inachukulia makubaliano ya ardhi ya Ukraine kuwa ni jambo lisiloepukika – suala hili la maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ni kubwa, kwani iwapo Ukraine ingekubali kutoa maeneo yake iliyotekwa kwa kukiuka sheria za kimataifa na Urusi, itapoteza uadilifu wake wa eneo. Hata hivyo, zaidi ya matokeo madhubuti yanayoweza kutokea ya mkutano huo, changamoto itakuwa ni kufuta kumbukumbu mbaya ya Februari 28 na kurekebisha uhusiano ulioharibiwa sana kati ya Ukraine na mshirika wake mkuu.

Mshirika wa kihistoria wa Marekani, Riyadh inaimarisha ushawishi wake wa kimataifa kwa mkutano huu, linaandika shirika la habari la AFP. Baada ya kupokelewa na Mwanamfalme, Volodymyr Zelensky amehakikisha kwamba atayashughulikia majadiliano ya Jumanne kwa njia “ya kujenga kabisa”, ikizingatiwa kwamba Saudi Arabia ilitoa “jukwaa muhimu sana la kidiplomasia.” Kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Ukraine, mkutano wao umelenga “upatanishi unaowezekana wa Saudi Arabia kwa ajili ya kuachiliwa kwa wafungwa wa kijeshi na raia na kurudi kwa watoto waliofukuzwa”, pamoja na dhamana ya usalama inayodaiwa na Kyiv.

Kyiv kukubali shingo upande

Majadiliano haya yanafanyika wakati ambapo Kyiv inajitahidi kwenye mstari wa mbele. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Urusi ilidai kufanya maendeleo makubwa katika eneo lake la Kursk na hata kusonga mbele katika eneo la Sumy la Ukraine, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2022. Siku ya Jumatatu, Machi 10, kamanda mkuu wa jeshi la Ukraine alitangaza kwamba Kyiv “itaimarisha” vikosi vyyake katika eneo la Kursk la Urusi. Kwa kuongezea, shambulio “kubwa” la makumi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine zililenga Moscow usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, amesema meya wa mji mkuu, Sergei Sobyanin.

“Ulinzi wa anga wa Wizara ya Ulinzi unaendelea kuzima shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani za adui zinazolenga Moscow,” Sobyanin almesema kwenye Telegram, akibainisha kuwa angalau drones 58 zilinaswa. Gavana wa Mkoa wa Moscow Andrei Vorobiov ameripoti kifo cha mtu mmoja na watatu kujeruhiwa katika shambulio hilo katika miji miwili katika vitongoji vya kusini mwa mji mkuu huo. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo umesitisha shughuli zake huku viwanja vingine vitatu vya ndege vinavyohudumia Moscow, Domodedovo, Zhukovsky na Sheremetyevo, “vimetekeleza vikwazo vya muda,” amesema Rosaviatsia, shirika la shirikisho la anga la Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *