Ukraine: Trump atangaza mazungumzo na Putin, Kyiv ina mashaka juu ya kusitishwa kwa mapigano

Wakati Donald Trump ametangaza kuwa atakutana na Vladimir Putin leo, Jumanne, Machi 18 – tangazo lililothibitishwa na Kremlin – kuhusu Ukraine na inaamini kuwa ina nafasi nzuri ya kufanya mazungumzo ya kumaliza vita nchini Ukraine, kwa upande wa Ukraine, ikiwa Kyiv itaonyesha nia ya kukubaliana na usitishaji wa mapigano. Hata hivyo watu wachache ndio wanakubali pendekezo hilo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Kremlin imethibitisha siku ya Jumatatu kwamba Marais wa Urusi na Marekani Vladimir Putin na Donald Trump watazungumza kwa simu siku ya Jumanne, ikiwa ni mara ya pili rasmi tangu kiongozi huyo kutoka chama cha Republican arejee Ikulu ya White House mwezi Januari. “Mazungumzo haya kwa kweli yanatayarishwa,” msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov amesema katika mkutano wa kila siku.

Kulingana na msemaji wa Kremlin, hali ya Ukraine itakuwa moja tu ya mada zilizojadiliwa na watu hao wawili. Dmitry Peskov amebainisha kuwa mkutano huu, wa pili katika miezi miwili, utajitolea hasa kufufua uhusiano kati ya Washington na Moscow. Njia ya kutoonyesha malengo madhubuti iwapo mijadala itageuka kuwa mbaya.

Hata hivyo kinachojulikana ni kwamba mazungumzo hayo yanatarajiwa kulenga udhibiti wa maeneo yaliyotekwa na majeshi ya Urusi katika ardhi ya Ukraine, pamoja na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, ambacho kinadhibitiwa na Moscow. Ingawa waangalizi wengi nchini Urusi wanachukulia mazungumzo hayo kuzaa matunda kutokana na kwamba viongozi hao wawili wanazungumza, hata hivyo wanatatizika kuelewa ni nini matokeo halisi ya majadiliano haya. Wala hawaoni azimio la haraka kwenye upeo wa macho, angalau sio haraka kama Donald Trump anataka.

Na wanataja sababu rahisi sana. Ukweli kwamba Washington ina jukumu la mpatanishi kati ya Moscow na Kyiv kutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili. Kwa macho yao, jambo pekee ambalo linaweza kutajwa mwishoni mwa mkutano huu litakuwa, kiwango cha utangamano kati ya misimamo ya Urusi na Marekani.

Wakati wa muhula wa kwanza wa Donald Trump, marais hao wawili walionyesha ukaribu fulani, wakikutana ana kwa ana mara tano. Mazungumzo yao yanayokumbukwa zaidi yalifanyika mnamo mwaka 2018 huko Helsinki, na moja kwa moja yalidumu zaidi ya masaa mawili. Muktadha ulikuwa uchunguzi wa uwezekano wa Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwaka 2016.

Miaka saba baadaye, uhusiano huu tete na wa ajabu ulirudi kwenye uangalizi na sauti imebadilika. Donald Trump, ambaye kwa muda mrefu alivutiwa na kiongozi huyo wa Urusi, anaonekana kukumbatia wazi msimamo wake. Wengine wanazungumza juu ya kupitishwa kwa sera zake kwa kuonyeshwa kwa kudharau sheria za kimataifa, matarajio ya ubeberu mamboleo, au hata ibada ya utu. Vladimir Putin alitangaza kwamba ikiwa Donald Trump angebaki madarakani mnamo mwaka 2020, kusingekuwa na vita nchini Ukraine. Je, Ukraine itawaleta watu hao wawili karibu zaidi au kuwatenganisha? Trump amefanya mapatano hayo kuwa ya heshima, lakini rais wa Urusi bado anapinga.

Hakuna udanganyifu kwa upande wa Kyiv

Nchini Ukraine, hakuna dhana potofu kuhusu usitishaji mapigano ambao Kyiv inataka, anaripoti mwandishi wetu wa Kyiv, Emmanuelle Chaze. Siku chache zilizopita, Volodymyr Zelensky alikumbusha kwamba hakukuwa na uaminifu kati yake na rais wa Urusi. Hii inaonyesha hali ya raia wa Ukraine, ambao wamekuwa na shida baada ya miaka mitatu ya vita kamili.

Kwa zaidi ya miaka kumi na moja,raia hawa wamekuwa na fursa ya kuona ukiukaji wa mikataba na makubaliano yaliyofanywa na Urusi kwenye ardjhi ya Ukraine. Lakini Kyiv pia inasubiri kuona kama Donald Trump atapata makubaliano kutoka upande wa Urusi, kwa kuwa baadhi ya matakwa ya Moscow hayakubaliki kwa sasa upande wa Ukraine, kama vile kuondolewa kwa wanajeshi au kusitishwa kwa maeneo ambayo bado hayajachukuliwa na Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *