Ukraine na Urusi, zimelaumiana kwa kuvunja mkataba wa saa 30 wa kusitisha vita kipindi cha Pasaka, mpango uliotangazwa na rais Vladimir Putin, Jumamosi iliyopita.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Rais Volodymyr Zelensky, amesema wanajeshi wa Urusi, walikiuka mkataba huo mara zaidi ya Elfu tatu, tangu ulipotangazwa na Putin kwa kutekeleza mashambulio kwenye ardhi ya Ukraine.
Urusi imeshtumiwa na Ukraine kwa kurusha makombora zaidi ya 1800 kwenye maeneo mbalimbali, huku rais Zelensky, akisema tangazo la Putin likikuwa maneno matupu kujaribu kufurahisha umma.
Urusi kwa upande wake nayo inasema, wanajeshi wa nchi yake, waliheshimu mkataba huo na kuishtumu Ukraine kwa kutumia makombora kutoka Marekani, kuishambulia.

Dmitry Peskov, msemaji wa Putin, amesema muda wa usitishwaji wa vita wakati wa kipindi cha pasaka, umekamilika na hautaongezwa.
Katika hatua nyingine, rais wa Marekani Donald Trump, amesema anatumai kuwa, mkataba wa kusitisha vita, kati ya Ukraine na Urusi, utapatikana wiki hii.
Trump ameongeza kuwa, iwapo mkataba huo utatiwa saini, Marekani itafanya biashara kubwa na mataifa hayo mawili.