
Urusi na Ukraine zimekubaliana kusitisha mashambulio ya kwenye bahari nyeusi na miundombinu ya nishati, makubaliano ambayo sasa yatatoa ahueni katika usafirishaji wa nafaka.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Makubaliano haya ambayo ni ya kwanza ya msingi kwa Urusi kukubali, yaliratibiwa na Marekani wakati huu Rais Donald Trump akishinikiza kumalizika kwa haraka kwa vita vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu nchini Ukraine.
Katika taarifa ya Ikulu ya White House, imesema kila nchi “ilikubali kuhakikisha kunakuwa na usafirishaji salama na kuzuia matumizi ya vyombo vya kibiashara kwa madhumuni ya kijeshi katika bahari hiyo.”
Hata hivyo licha ya kukubaliana kuhusu mpango huu, Urusi inasema makubaliano haya yataweza kutekelezwa pale tu nchi hiyo itakapoondolewa vikwazo katika sekta yake ya kilimo.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye amegeukia diplomasia baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa Trump, amesema ni mapema mno kusema ikiwa makubaliano hayo yataheshimiwa na Moscow.