Ukraine: Milipuko yaikika katika kyiv, ‘mashambulio ya makombora’ yanaendelea (meya)

Wahudumu wa afya wametumwa katika wilaya mbili za Kyiv kufuatia milipuko na “mashambulio ya makombora” amba yo bado yanaendelea, meya wa mji mkuu wa Ukraine, Vitali Klitschko, amesema leo Jumapili asubuhi, Aprili 6. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Klitschko amethibitisha kuwa ulinzi wa angani umeanzishwa na kuhimiza wakaazi kuwa katika maeneo salama. 

Kunasikika milipuko katika mji mkuu. Ulinzi wa anga unafanya kazi. “Kaeni maeneo salama!” meya ametangaza kwenye Telegram. “Mahambulio ya makombora dhidi ya Kyiv yanaendelea,” meya wa Kyiv ameandika bila kutoa maelezo zaidi, shirika la habari la AFP limeripoti.

Takriban watu watatu wmejeruhiwa katika shambulio hilo, ambalo linakuja siku mbili baada ya shambulio linginelililoua watu 18, nusu yao wakiwa watoto.

Diwani wa jiji ametangaza kwanza kwenye Telegram kwamba kulikuwa na “milipuko katika mji mkuu” na “mashambulio ya makombora katika mji wa Kyiv” lilikuwa linaendelea. Kisha ameripoti angalau watu watatu “wamejeruhiwa” katika wilaya tatu za mji mkuu.

Wakati huo huo, mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine umetoa tahadhari kwa mikoa ya Kharkiv, Mykolaiv na Odessa kutokana na “makombora ambayo yalikuwa yamepenya eneo la Chernihiv kutoka kaskazini na kuelekea kusini.” Tahadhari hizi zote ziliondolewa baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *