Ukraine kupata msaada ‘Muhimu’ wa Marekani mwishoni mwa Septemba

Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan
alizungumza kwa njia ya video kwenye mkutano wa Mkakati wa Ulaya wa Yalta na
kukiri kucheleweshwa kwa vifaa vya kijeshi kwa Ukraine.

“Hili si suala la utashi wa kisiasa,” alielezea. “Hili ni suala la kuondokana na ugumu
wa ugavi wa vifaa.” “Lakini kutokana na kile Ukraine inachokipinga,
tunahitaji kufanya zaidi na kuifanya vizuri zaidi,” Sullivan aliongeza. Alitangaza
kifurushi kipya cha msaada “muhimu” mwishoni mwa mwezi.