
Viongozi wa Marekani na Ukraine wamekubaliana kukutana nchini Saudi Arabia mwanzoni mwa juma kujaribu kupata msimamo wa pamoja kabla ya mazungumzo yajayo kati ya Washington na Moscow ili kumaliza vita nchini Ukraine.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Wakati ujumbe wa Marekani utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, ujumbe wa Ukraine utaongozwa na Rais Volodymyr Zelensky, ambaye anatazamiwa kukutana na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman siku ya Jumatatu, Machi 10.
Baada ya kufanya mfululizo wa mazungumzo, haswa na wenzake wa Umoja wa Ulaya, EU, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Ulaya huko Brussels, rais wa Ukraine anasema ana imani katika mkesha wa majadiliano ambayo yanatarajiwa kufanyika Jumanne 11 Machi kati ya ujumbe wa Marekani na ule wa Ukraine huko Saudi Arabia. Ukraine “inataka” amani na Urusi ndiyo “sababu pekee ya vita kuendelea,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo Jumatatu, Machi 10, katika mkesha wa mazungumzo haya ambayo yanaweza kuwa muhimu.
Kwa mkutano huu wa kwanza na utawala wa Trump, Volodymyr Zelensky, ambaye anatarajiwa kukutana na Mwanamfalme Mohammed Ben Salman atakapowasili Saudi Arabia leo Jumatatu Machi 10, atasindikizwa vyema. Kama alivyotangaza mwishoni mwa juma hili lililopita, ujumbe wake utaundwa na mshauri wa rais Andriy Yermak, mkuu wa diplomasia, Waziri wa Ulinzi na naibu mkurugenzi wa ofisi ya rais, pamoja na maafisa mbalimbali wa ngazi za juu wa jeshi. Mkuu wa nchi ya Ukraine, ambaye hatashiriki moja kwa moja katika majadiliano hayo, amewachagua wajumbe wake wanaoaminika zaidi kujaribu kupata dhamana ya usalama kutoka Marekani kabla ya uwezekano wa kusitisha mapigano na Urusi.
Jumbe wa Huruma
Lakini baada ya kipindi cha mkutano katika Ikulu ya White House na Donald Trump na Makamu wa Rais J. D. Vance wakati ambao Volodymyr Zelensky alidhalilishwa hadharani, shughuli hiyo inaonekana dhaifu. Hii ndiyo sababu, tangu tukio hili, rais wa Ukraine amekuwa akijaribu kutuma jumbe za huruma kwa Washington ili kupunguza mvutano huo. Katika hotuba kuhusu ukosoaji aliopokea kwa mavazi ya kijeshi ambayo amekuwa amevaa tangu kuanza kwa mzozo wakati wa ziara yake ya hivi majuzi huko Washington, rais wa Ukraine hata ameomba radhi – kwa kutojitokeza “amevaa mavazi ya kiraia” kwenye sherehe huko Kyiv Jumapili, Machi 9.
Katika mkesha wa kufunguliwa kwa mazungumzo, msimamo wa Kyiv unabaki kuwa ule ule sawa na Umoja wa Ulaya: ili mkataba wa amani utiwe saini kwa lengo la kumaliza vita na Urusi, mkataba huo unapaswa kuwa wa haki na wa kudumu.
Ujumbe wa Marekani utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, ambaye pia ataandamana na maafisa kadhaa wa kidiplomasia na kijeshi.