
Waziri wa ulinzi wa Ukraine, Rustem Umerov, amesema mazungumzo ya kutafuta amani kati ya ujumbe wa Marekani na Ukraine jijini Riyadh, Saudi Arabia, yamelimazika vyema, leo ikiwa zamu ya Urusi kuhusishwa kwenye mazungumzo hayo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa Waziri Umerov, mazungumzo kati ya ujumbe wake na ule wa Marekani yalijikita kwenye maswala ya kawi, na kulinda miundo mbinu ya Ukaine.
Baadaye leo mazungumzo hayo yatajumuisha ujumbe kutoka Urusi, yote haya ikiwa chini ya juhudi zinazooongozwa na rais wa Marekani, Donald Trump, kutafuta amani ya Kudumu nchini Ukraine.
Licha ya juhudi zinazoendelea za kumaliza vita nchini Ukraine, pande zote zimeripotiwa kuendeleza mashambulio, rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, akimtuhumu rais wa Urusi, Vladimir Putin, kwa kuendeleza mashambulio akidai Urusi ndio inayochelewesha kupatikana kwa amani na nisharti ushurutishe kumaliza vita.
Rais Putin amekataa pendekezo la kusitisha vita kwa siku 30, na badala yake amependekeza vituo vya nishati visishambuliwe.