Ukraine: Emmanuel Macron aonya dhidi ya amani ambayo itakuwa ‘kujisalimisha’

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameonya kwamba amani itakuwa sawa na “kujisalimisha” kwa Ukraine na kuhoji kama mwenzake wa Urusi Vladimir Putin “yuko mwaminifu” tayari kwa usitishaji mapigano “wa kudumu” katika mahojiano na Gazeti la Financial Times yaliyorushwa leo Ijumaa (Februari 14, 2025).

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Amani ambayo ni usaliti ni habari mbaya kwa kila mtu,” amesema kwa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ana nia ya kuingia katika mazungumzo moja kwa moja na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin. “Swali pekee katika hatua hii ni: ‘Je, Rais Putin ni mwaminifu, endelevu, na kwa njia endelevu tayari kwa usitishaji vita kwa msingi huu?’ “, amebainisha mkuu wa nchi wa Ufaransa. Emmanuel Macron pia amebainisha kuwa Ukraine “pekee” inaweza “kujadiliana na Urusi” kile kinachohusu uhuru wake na uadilifu wa eneo.

Waziri mpya wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth siku ya Jumatano aliona kuwa  “si sahihi” kuzingatia Ukraine kurudi kwenye mipaka yake ya kabla ya 2014. Urusi, ambayo ilitwaa eneo la Crimea mwaka 2014, inachukulia kama sehemu yake mikoa mitano iliyochukuliwa kwa viwango tofauti tangu kuanza kwa mashambulizi yake nchini Ukraine mwezi Februari 2022.

Rais wa Ufaransa pia amesisitiza katika Gazeti la Financial Times juu ya haja ya Umoja wa Ulaya kuwa kwenye meza ya mazungumzo juu ya usanifu wa usalama wa baadaye wa bara hilo. “Ni juu ya jumuiya ya kimataifa, pamoja na jukumu maalum kwa Umoja wa Ulaya, kujadili dhamana ya usalama na, kwa upana zaidi, sheria za usalama kwa eneo zima. Hapa ndipo tunaposema kwamba tuna jukumu,” amebaini rais wa Ufaransa.

Emmanuel Macron alikuwa wa kwanza kutaja kutuma wanajeshi wa nchi kavu nchini Ukraine ili kuhakikisha usalama wake kutoka kwa Urusi endapo kutakuwa na usitishaji mapigano. Mkuu wa Pentagon amesisitiza kwamba itakuwa juu ya Umoja wa Ulaya kupata dhamana “imara” ya usalama kwa ajili ya kudumisha amani “ya kudumu”, akikifuta hoja ya kutumwa kwa wanajeshi wa Kimarekani nchini Ukraine.