Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu umeripotiwa katika maeneo yanayokaliwa na M23

Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaripotiwa katika maeneo yanayokaliwa na waasi wa M23 katika mkoa wa Kivu Kusini, hasa katika mji wa Bukavu. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanashutumu mauaji, wizi, ubakaji na uporaji unaofanywa na waasi, hivyo kusababisha hofu miongoni mwa watu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Radio OKAPI, watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, waliuawa mchana kweupe mbele ya wakazi siku ya Jumamosi, Machi 13. Kulingana na mashahidi, wahasiriwa walikataa kuandikishwa kwa kulazimishwa na M23, kundi lenye silaha linaloungwa mkono na jeshi la Rwanda ambalo linamiliki eneo hilo. Raia wawili waliuawa hadharani: mmoja katika wilaya ya Kadutu na mwingine katika eneo la Walungu. Hata hivyo, maafisa wawili wa polisi waliuawa kwa kupigwa risasi, mmoja katika wilaya ya Cimpunda na mwingine katika kambi ya Jules Moke iliyoko Bagira, mjini Bukavu.

Vitendo hivi vimeibua hasira kali miongoni mwa mashirika ya haki za binadamu, ambayo yanaeleza kuwa ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu.

Tangu M23 ilipochukuwa udhibiti wa mji wa Bukavu tarehe 15 Februari, mashirika ya kiraia katika mkoa wa Kivu Kusini yamerekodi takriban kesi sitini za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Vitendo hivi ni pamoja na mauaji ya kinyama, ukatili wa kijinsia, uporaji na visa vya watu kutoweka.

Katika taarifa iliyochapishwa Jumamosi, Machi 13, mashirika ya kiraia pia yalifichua kuwepo kwa makaburi ya halaiki kando ya Mto Ruzizi, kwenye mpaka kati ya DRC na Rwanda.

“Vitendo hivi vinajumuisha ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu ambavyo vinapaswa kuadhibiwa,” mashirika hayo yamesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *