Ukingo wa Magharibi, uwanja mpya baada ya Ghaza wa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

Kufuatia kusitishwa mapigano katika maeneo ya kusini mwa Lebanon na Ukanda wa Ghaza, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeanzisha operesheni mpya katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Operesheni hiyo ambayo malengo yake halisi hayajatajwa, imezusha wasiwasi kutokana na kuendelea kwake sambamba na tangazo lililotolewa na Trump la kutaka Wapalestina wa Ghaza wahamishiwe katika nchi za Misri na Jordan.