
UNICEF kwa mara nyingine tena IMEtoa wito wa kukomeshwa kwa uhasama na kuanzishwa kwa usitishaji mapigano Gaza. Shirika la Umoja wa Mataifa linalosaidia watoto linasikitishwa na kuanza tena kwa mashambulizi ya mabomu na operesheni ya ardhini na jeshi la Israeli tangu Machi 18. Mashambulizi ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 300 miongoni mwa watoto, wengi wao wakiwa wamekimbia makazi yao.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mnamo Machi 18, jeshi la Israeli lilianzisha mashambulizi 100 kwa wakati mmoja katika Ukanda wa Gaza, na kumaliza usitishaji wa mapigano na Hamas. Katika chini ya saa 48, mamia ya watu waliuawa, ikiwa ni pamoja na angalau watoto 183.
Tangu Machi 18, jumla ya watoto 322 wameuawa katika mashambulizi makali ya jeshi la Israeli, kulingana na UNICEF.
Wengi wao walikuwa watu waliohamishwa na kupelekwa katika maeneo yaliyotolewa kama makazi katika mahema au majengo yaliyoharibiwa. Huko Al-Mawasi, kusini mwa Gaza, kwa mfano, eneo hilo hupigwa makombora mara kwa mara na jeshi la Israeli.
Watoto walipoteza maisha wakati wa sherehe za Eid
Katika kipindi hicho, watoto wengine 609 walijeruhiwa, kulingana na shirika hilo la Umoja wa Mataifa. Siku ya Jumapili, tena, watoto waliuawa huko Khan Younes wakati wa kusherehekea Eid.
Hata hivyo, tangu Machi 2, hakuna msaada ulioruhusiwa kuingia Gaza. Wavu wa usalama ambao watoto wanahitaji sana kwa kula na kupata huduma za matibabu, UNICEF inasisitiza.
UNICEF inaendelea kutoa wito kwa pande husika “kusitisha uhasama na kuanzishwa tena usitishaji mapigano na kuheshimu wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu ya kuwalinda watoto.”