UJUMBE WA TANZANIA WASHIRIKI VIKAO NA BENKI YA DUNIA KUHUSU MIRADI YA MAENDELEO

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, umeshiriki katika vikao muhimu na Benki ya Dunia vilivyofanyika leo Aprili 22, 2025, jijini Washington, Marekani. Vikao hivyo vimejikita katika kujadili upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Wajumbe wengine walioambatana na Mhe. Waziri ni Bw. Stanslaus Nyongo, Naibu Waziri wa Mipango na Uwekezaji; Dkt. Fred Msemwa, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango; Bw. Emmanuel Tutuba Gavana wa Benki Kuu Tanzania; Dkt. Natu Mwamba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha; na Bw. Adriano Ubise. Ushiriki wa ujumbe huu ni sehemu ya jitihada za Serikali kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

The post UJUMBE WA TANZANIA WASHIRIKI VIKAO NA BENKI YA DUNIA KUHUSU MIRADI YA MAENDELEO appeared first on Mzalendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *