
Afisa wa Hamas ameliambia shirika la habari la AFP kwa maofisa wa ngazi ya juu wa kundi hilo wanaelekea jijini Cairo leo Jumamosi kwa mazungumzo ya usitishwaji wa mapigano katika Ukanda wa Gaza na wapatanishi wa Misri.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na afisa huyo ambaye yuko karibu na mazungumzo hayo, Hamas ina matumaini kwamba makutano huu utasaidia katika upatikanaji wa makubaliano ya kumaliza mapigano na kuondoka kwa wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Ujumbe maalum wa Hamas utaongozwa na mpatanishi wake mkuu Khalil al-Hayya.
Aidha mjumbe huyo amesema, Hamas haijapokea mapendekezo yoyote mapya kuhusiana na usitishaji wa mapigano licha ya vyombo vya habari vya Israel kueleza kwamba Israel na Misri zilikuwa zimebadilishana stakabadhi zinazoangazia uwezekano wa kusitishwa kwa mapigano na kuachiwa kwa mateka.
Hamas inaendelea kuituhumu Israel kwa kuendelea na uvamizi katika Ukanda wa Gaza licha ya kwamba wapatanishi wa kila pande wanaendelea kuwasiliana.