Ujue Mfumo wa Kisasa wa Iran wa Bavar 373 uliotumika kuzima hujuma ya Israel

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika Makala hii ambayo huangazia baadhi ya matukio muhimu ya sayansi nchini Iran na maeneo mengine duniani. Leo Makala yetu maalumu itaangazia mfumo wa kujihami angani wa Iran ujulikanao kama Bavar 373 ambao uwezo wake mkubwa umewashangaza wengi duniani.

Mwezi uliopita wa Oktoba, Kamandi ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitangaza kwamba vikosi vya ulinzi wa anga vya Iran vilitungua kwa mafanikio idadi kubwa makombora ya Israel. Aidha mfumo huo wa kujihami angani ulizuia ndege za kijeshi za utawala huo haramu wa Israel kupenya kwenye anga ya Iran wakati wa shambulio la hivi karibuni.

Kamandi hiyo ilitangaza kwamba ndege za kivita za Israel zilirusha makombora ndani ya ardhi ya Iran  kinyume cha sheria za kimataifa mapema Jumamosi, Oktoba 26, 2024.

Taarifa zinasema ndege za utawala haramu wa  Israel, zikiwemo zile za kisasa kabisa za F-35,  zilitumia kituo cha jeshi la kigaidi la Marekani  nchini Iraq, kilicho umbali wa kilomita 100 kutoka mpaka wa Iran na kuvurumisha makombora kadhaa ya masafa marefu ya angani hadi nchi kavu katika mikoa ya Ilam na Khuzestan na pia nje  kidogo ya mkoa wa Tehran.  

Kikosi cha ulinzi wa anga za Iran kilitungua karibu makombora yote yaliyovurumishwa na ndege za kivita za Israel kwa kutumia mfumo wa kisasa wa ulinzi wa angani ulioundwa ndani ya nchi. Wataalamu wa kijeshi wanasema moja kati ya mifumo wa ulinzi wa anga Iran iliyootumika kuzima uchokozi huo wa Israel ni ule ujulikanao kama Bavar-373.

Mashambulizi hayo ya Israel yalizimwa na hayakusababisha hasara kubwa kama Wazayuni walivyokusudia na hilo lilitokana na teknolojia ya mfumo huo wa kujihami angani wa Iran.

Ndege za kisasa kabisa za kivta za Marekani ain ya F-35 ambazo zilishindwa kupenya kwenye anga ya Iran kutokana na kuwepo mfumo wa kujihami angani wa Bavar 373

Baadhi ya nukta muhimu za mfumo wa Bavar-373

Mfumo wa ulinzi wa anga wa  Bavar-373,  ni mojawapo ya mifumo yenye uwezo mkubwa zaidi duniani katika ulinzi wa anga. Mfumo huu ulianza kutumika mwaka 2020 na ni matokeo ya juhudi za miaka kumi za wataalamu wa Iran.

Mfumo huu hutumiwa kuwinda aina mbalimbali za shabaha, ikiwa ni pamoja na makombora ya cruise, ndege zisizo na rubani na ndege za kizazi cha tano zisizoonekana kwenye rada, katika miinuko ya chini na juu.

Bavar ni neno la Kiajemi lenye maana ya imani, na 373 ni jumla ya herufi za Abjad za neno Mohammad, jina la Mtume Mtukufu wa Uislamu (SAW).

Wataalamu wa kijeshi wanasema  mfumo wa ulinzi wa angani wa Bavar-373 unaweza kulinganishwa na ule wa Russia wa S-400 na ule wa Marekani wa Patriot na pia THAAD.

Mfumo wa Bavar-373 ulianzishwaje?

Haja ya mfumo wa ndani wa ulinzi wa anga wa masafa marefu ilionekana mnamo 2010 wakati Russia, chini ya mashinikizo ya Marekani  wakati huo, ilisimamisha mpango wa kuiuzia Iran  mfumo wa makombora ya ulinzi wa angani ya S-300 PMU-1.

Muundo wa awali wa  mfumo wa Bavar-373 ulionyeshwa hadharani mwishoni mwa 2011 na ulielezewa na maafisa wa jeshi kuwa wa hali ya juu zaidi kuliko ule wa S-300 wa Russia .

Mwaka huo huo, Iran iliunda trela maalumu ijulikanayo kama Zoljanah 10X10 inayotumiwa  kubeba makombora ya mfumo huo wa Bavar-373.

Lori aina ya Zoljanah 10X10

Mnamo mwaka wa 2014, katika hafla mbalimbali za kijeshi, Iran ilizindua aina mpya trela hiyo yenye uwezo wa kutumiwa kubeba mfumo makombora  wa Bavar-373.

Mwaka mmoja baadaye, baada ya kutiwa saini makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuondolewa vikwazo, Russia ilitangaza kuwa itaipatia Iran mfumo wa S-300 PMU-2. Pamoja na kuwa Iran ilikubali kutumia mfumo huo wa kigeni lakini iliendelea kuboresha mfumo wake wa Bavar-373.

Katikati ya mwaka wa 2015, Waziri wa Ulinzi wa wakati huo alitangaza kwamba Iran imekamilisha uundwaji wa mfumo wa  Bavar-373 ulioundwa kikamilifu nchini, huku uzalishaji kwa wingi ukianza muda mfupi baadaye.

Pia alisema kuwa Iran haitanunua mfumo wa makombora wa ulinzi wa anga wa S-400 uliotengenezwa Russia, ingawa Moscow ilikuwa imejitolea kuiuzia.

Kizazi mpya

Mwishoni mwa 2022, kizazi kipya cha mfumo wa Bavar-373 kilizinduliwa, kikiwa na rada zenye uwezo zaidi na kombora jipya za la Sayyad-4B lenye masafa marefu kuliko ya awali.

Mfumo wa Bavar-373 una sehemu kadhaa. Unajumuisha mitambo ya kurusha makombora pamoja na rada.

Pia ni mfumo unaoweza kuhamishwa haraka kwani mtambo wake wote unaweza kubebwa kwenye treal maalumu ya Zoljanah.

Mfumo wa  Bavar-373 unaweza kujumuisha treal sita maalumu za Zoljanah, zilizoegeshwa kwa karibu. Mfumo huo unaweza kuwa na makombora hadi 24 katika eneo moja.

Mfumo wa Bavar-373 hutumia makombora ya aina ya Sayyad-4B, yenye masafa ya kilomita 300.

Mfumo wa Bavar 373 una rada kubwa aina ya Meraj-4 ambayo ina muundo wa  3D S-Band AESA .

Kazi yake ni kudhibiti eneo la anga lenye upana wa zaidi ya kilomita za mraba 636,000 na kutoa taarifa kwa mifumo ya ulinzi iliyo karibu nayo.

Rada aina ya Meraj -4 

Mpangilio wa mwongozo wa mawimbi wa Meraj-4 na kipimo data cha 250 MHz huzunguka kutoka mara 3 hadi 6 kwa dakika na hivyo rada hiyo inaweza kutambua chombo chochote chenye yenye kasi ya hadi Mach 3 (Kilomita 3 675 kwa saa), na linaweza kulenga shabaha kuanzua  kuanzia urefu wa mita 100 hadi kilomita  25 km katika eneo lenye umbali wa hadi kilomita 450.

Mbali na rada ya Meraj-4, mfumo wa Bavar-373 pia hutumia rada ya Hafez S-band AESA, inayobebbwa na lori aina ya Zafar 8×8, ambayo ina upeo wa juu wa kilomita 300 na uwezo wa kugundua shabaha 100 kwa wakati moja.

Hayo ni maelezo mafupi tu kuusu mfumo wa ulinzi wa anga wa Bavar-373 ambao ni miongoni mwa mifumo ya kujihami angani ya Iran. Maelezo mengine mengi ni ya siri na hayawezi kutangazwa.