
Baada ya Uingereza na Canada, Ujerumani imetangaza siku ya Jumanne Machi 4, 2025 kwamba itakatiza msaada wake mwingine kwa Rwanda ili kukabiliana na mashambulizi ya M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Tutasitisha ahadi mpya za kifedha na mikutano ya ngazi ya juu na Kigali na kupitia upya ushirikiano uliopo na Rwanda.” Wizara ya Ushirikiano ya Ujerumani ilmetangaza uamuzi wake katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumanne, Machi 4, anaripoti mwandishi wetu huko Berlin, Pascal Thibaut. Ujerumani inalaani mashambulizi ya kundi la M23 na kulaani “ukiukaji wa uadilifu wa eneo na mamlaka ya DRC“.
Berlin hapo awali iliarifu Kigali, ambayo inapokea msaada wa kila mwaka wa euro milioni 50 kwa mwaka kwa ajili ya miradi inayohusiana na maendeleo ya kiuchumi, nishati, ulinzi wa tabianchi au uzalishaji wa chanjo.
Soma piaHali ya usalama mashariki mwa DRC katikati mwa ziara ya Félix Thisekedi nchini Ujerumani
Katika mazungumzo yake na Kigali, Berlin kwa mara nyingine tena imedai kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda nchini DRC na kukomesha uungaji mkono wa M23. “Wakati wa mkutano huo, ilisisitizwa pia kwamba masuala ya usalama wa Rwanda lazima yachukuliwe kwa uzito na kwamba Ujerumani pia iliwasiliana na upande wa Kongo kuhusu suala hili,” wizara ya Ujerumani imeongeza.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda imejibu kwa kusema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba “usiasa” wa Ujerumani wa ushirikiano wa kimaendeleo ulikuwa “mbaya na hauna tija.”
Mwishoni mwa mwezi wa Januari, Berlin ilikuwa tayari imeamua kufuta mashauriano ya serikali na Rwanda.
Mnamo Februari 25, London ilitangaza kuwa inasitisha misaada yake mingi ya kifedha kwa Rwanda. Siku ya Jumatatu, Ottawa ilitangaza kuwa “itasimamisha utoaji wa vibali vya kusafirisha bidhaa na teknolojia zilizotakiwa kwenda Rwanda,” pamoja na miradi mipya ya kiuchumi ya serikali, na kupitia upya ushiriki wake katika hafla za kimataifa zilizoandaliwa nchini Rwanda.