
Kulingana na Shirika la Waandishi Wasio na Mipaka (RSF), faharisi ya uhuru wa vyombo vya habari duniani inaonyesha kushuka kwa jumla kwa hali ya kazi ya wanahabari na katika upatikanaji wa habari bora za kujitegemea kwa umma katika ngazi ya kimataifa.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Nusu ya nchi 180 katika orodha ziko katika orodha nyekundu, ikimaanisha kuwa ziko katika hali ngumu au hata mbaya sana – kiwango muhimu ambacho hakijawahi kushuhudiwa, kulingana na RSF. Vikwazo vikuu vya uhuru wa vyombo vya habari: usalama, mambo ya kisiasa na kiuchumi.
Unyanyasaji wa kimwili dhidi ya waandishi wa habari ni vikwazo vinavyoonekana zaidi kwa uhuru wa vyombo vya habari. Katika maeneo ya migogoro – huko Gaza, Ukraine, Sudani au Sahel – waandishi wa habari wanauawa, wanafungwa, wanazuiwa kufanya kazi au kulazimishwa kukimbilia uhamishoni.
“Eritrea inasalia kuwa nchi ya mwisho katika orodha ya Shirika la Habari la Waandishi Wasio na Mipaka (RSF) duniani, ikiwa na vyombo vya habari ambavyo havipo kabisa leo, na waandishi wa habari kama Dawit Isaak, ambaye ni mwandishi wa habari aliyefungwa kwa muda mrefu zaidi duniani bila kufunguliwa mashitaka. Tunaona baadhi ya nchi ambazo ziko kwenye orodha ya juu kama vile Uganda, Rwanda na Ethiopia. “Pia tunaona hali ambayo ni ya kudorora kwa hali ya usalama hasa nchini Sudani, pamoja na vyombo vingi vya habari ambavyo vimelazimika kufanyia kazi yao nje ya nchi, ” ameshutumu Anne Bocandé, mkurugenzi wa wahariri wa RSF, akizungumza na Sophie Malibeaux wa RFI.
“Pia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako, mashariki mwa nchi, waandishi wa habari wengi wamelazimika kuhama, kukimbia, na vituo vya redio vya ndani vimekaliwa na kulazimishwa kufungwa. Na ni wazi, katika eneo la Sahel, suala la usalama linaendelea kuibuka, na vyombo vya habari vya kigeni vikisitishwa, pamoja na waandishi wa habari wa ndani kuzuiwa. Tuliiona nchini Burkina Faso ikiwa na angalau waandishi wa habari wanne waliosajiliwa kwa nguvu katika jeshi, mwandishi wa habari aliyezuiliwa nchini Mali, na hali ambayo inazidi kulazimisha vyombo vya habari kujikagua,” anaongeza.
Hatua ya Marekani kuzuia misaada yake yasababisha athari
“Uhuru wa vyombo vya habari kwa kweli unazidi kuzorota. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10, tunaona kwamba hali ya wastani inaelekea katika hali ngumu. Hii ni ishara ya wasiwasi kwetu, kwa hakika. Katika hali halisi, hali ya kufanya kazi kama mwandishi wa habari ni duni katika nusu ya nchi duniani leo, na 0.7% ya watu duniani wanaishi katika nchi ambayo uhuru wa habari uko hatarini., amebaini Anne Bocandé.