
Sehemu kubwa ya Uhispania na Ureno zimeathiriwa na hitilafu kubwa ya umeme siku ya Jumatatu. Mamlaka ya umeme wa gridi ya Iberia Red Electrica imesema ilikuwa inafanya kazi na kampuni za nishati kurejesha umeme. Kukatika kwa umeme pia kumeathiri kusini mwa Ufaransa.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
E-Redes, kampuni ya ufuatiliaji wa umeme wa gridi ya Uhispania, imesema katika taarifa kwamba ilikuwa inafanya kazi kurejesha umeme hatua kwa hatua. “Hili ni tatizo pana la Ulaya,” kampuni hiyo imesema.
“Tunaanzisha mipango ya kurejesha usambazaji wa umeme kwa ushirikiano na makampuni katika sekta hiyo baada ya hitilafu ya umeme kutokea katika mfumo wa peninsula,” ametangaza meneja wa mtandao wa Red Electrica kwenye ukurasa wake wa X, akibainisha kuwa “sababu zinachunguzwa.”
“Tunaanza kurejesha umeme kaskazini na kusini mwa peninsula, jambo ambalo ni muhimu kukabiliana hata kwa hatua na usambazaji wa umeme,” Red Electrica pia imetangaza kwenye mtandao wa kijamii wa X katika awamu ya pili.
Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez yuko njiani kuelekea kituo cha udhibiti wa Mtandao wa Umeme wa Uhispania (REE), kulingana na ofisi yake. Kulingana na redio ya umma RNE, kukatika huko hakuathiri Visiwa vya Canary na Visiwa vya Balearic. “Kutokana na hitilafu ya umeme, baadhi ya matukio yalitokea katika viwanja vya ndege. “Jenereta za dharura zimewashwa,” amesema meneja wa uwanja wa ndege Aena kwenye myandao wa kijamii wa X.