Ugonjwa wa Chikungunya unazidi kuongezeka Reunion, mamlaka yatangaza kampeni ya chanjo

Katika kisiwa cha Ufaransa cha Réunion, ugojwa wa chikungunya umesababisha vifo vya kwanza: watu wawili wenye umri wa miaka 86 na 96 walifariki wiki iliyopita. Shirika la Afya la katika kisiwa hicho limebainisha siku ya Ijumaa, Machi 21, udharura wa kutanguliza chanjo kwa wazee na watu wazima wenye magonjwa mengine kufuatia idhini ya Umoja wa Ulaya ya chanjo ya kwanza. Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, watu 8,500 waliambukizwa virusi hivyo vinavyoenezwa na mbu.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Hii sio mara ya kwanza kwa Kisiwa cha Reunion kuathiriwa na janga hili: mnamo mwaka 2006, tarehe ya janga la hapo awali, theluthi moja ya watu waliambukizwa na watu 225 walifariki. Kwa mujibu wa mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko Antoine Flahault, virusi hivi mara nyingi huwa havina madhara, lakini vinaweza kuwa mbaya kwa wazee au walio katika mazingira magumu sana: “Neno chikungunya ni la Kiswahili, linamaanisha ‘kutembea umejikunja’.” Hii inamaanisha kuwa mgonjwa huwa ana maumivu makali ya viungo na hivo kushindwa kutembea. “

Virusi hivyo viligunduliwa mwaka wa 1952 nchini Tanzania, vinaenezwa na mbu wa chui, ambao wamekuwa wakifika kwa wingi katika miji ya Réunion katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita: “Baada ya kimbunga Garance kupiga hivi karibuni kisiwa hicho na joto kali ambalo limesababisha mbu hao kuongezeka kwa sasa,” anaeleza mtaalamu huyo wa magonjwa. Lakini tusisahau kwamba ni mbu wa nyumbani, nikimaanisha kwamba sisi ndio tunawafanya wazaane kwa wingi kwenye bustani zetu. Ni mbu aliye karibu na nyumba na ambaye mara nyingi huuma nje, sio ndani ya nyumba. “

Ni kwa kumuuma mtu aliyeambukizwa ndipo mbu hubeba virusi na kusambaza kwa kuuma mtu mwingine. Kwa hivyo virusi hivyo huenea haraka sana: “Hakuna sababu nyingi kwa nini visiwa vingine vinavyozunguka vinapaswa kuepukwa. Hili ni tatizo ambalo lazima sasa livihusu visiwa vyote vya Bahari ya Hindi. “

“Kunaweza kuwa na janga lingine kubwa kwenye Kisiwa cha Reunion.”

Antoine Flahault anaonyesha kwamba mlipuko wa janga daima ni sababu ya wasiwasi: “Hivi sasa, 1% ya wagonjwa hulazwa hospitalini na karibu mmoja kati ya elfu hufa. Virusi hivi mara nyingi huchukuliwa kuwa mbaya na hauhitaji majibu mengi. Kwa sasa tunafikia wagonjwa 3,000 kwa wiki, ambapo mwaka wa 2006, tuliona wagonjwa 45,000 kwa wiki katika kilele cha janga hilo. Kunaweza kuwa na janga lingine kubwa kwenye Kisiwa cha Reunion, na wakati huo, vyumba vya dharura vitajaa tena na kiwango cha vifo kitakuwa kikubwa. Kwa hivyo ugonjwa huu ambao tunaamini kuwa ni mbaya ni ugonjwa ambao lazima tuwe macho sana. “

Chanjo ya kwanza dhidi ya Chikungunya iliidhinishwa katika msimu wa vuli na Umoja wa Ulaya. Imetengenezwa nchini Ufaransa na Austria, itasambazwa kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa Aprili kwa walio na umri wa zaidi ya miaka 65 na kwa watu walio na magonjwa mengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *