Uganda: Museveni aagiza uchunguzi kuhusu vurugu wakati wa uchaguzi mdogo

Siku chache baada ya chama tawala nchini Uganda, NRM kutangaza kuyakataa matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye eneo la Kawempe, rais Yoweri Museveni, sasa ametangaza kuanza kwa uchunguzi kuhusu vurugu zilizojitokeza wakati wa uchaguzi huo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake aliyochapishwa kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, rais Museveni alisisitiza msimamo wa chama chake kuwa hwakubaliani na matokeo yaliyokipa ushindi chama cha upinzani cha NUP, akidai kulikuwa na udanganyifu.

Katika hali isiyo ya kawaida, rais Museveni anadai kuwa chama cha NUP kinachoongozwa na Bob Wine, kulivuruga uchaguzi huo katika baadhi ya vituo vya kupigia kura huku mawakala wake wakikamatwa na kura bandia.

Cha cha NUP chake Bobi Wine kiliibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo mdogo wa ubunge.
Cha cha NUP chake Bobi Wine kiliibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo mdogo wa ubunge. REUTERS – ABUBAKER LUBOWA

Kwenye chapisho lake, Museveni amehoji uhalali wa ushindi wa NUP akisema chama chake kimeenda mahakamani kupinga matokeo hayo, huku akiwazodoa watu waliohoji kwanini wanajeshi walitumika kuwadhibiti wanasiasa wa upinzani pamoja na wanahabari.

Hata hivyo kauli yake, imepokelewa kwa mshangao na wanaharakati wa demokrasia wanaodai kuwa kama uchaguzi ulivurugwa basi ulivurugwa na polisi na wanajeshi waliotumwa kwa makusudi kuwatisha wapiga kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *