
Serikali ya Uganda, inapanga kuwasilisha mswada bungeni, ili kupitisha sheria itakayoruhusu raia wa kawaida, kushtakiwa katika Mahakama za kijeshi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mpango huu unakuja, licha ya Mahakama ya Juu mwezi Januari, kupiga marufuku raia wa kawaida kushatakiwa kwenye Mahakama za kijeshi.
Waziri wa Sheria, Nobert Mao, amesema mswada huo uko tayari, na sasa unasubiri kupitishwa na Baraza la Mawaziri, kabla ya kuwaislishwa bungeni.
Mao amesema, mswada huo, umeeleza baadhi ya mashtaka ambayo, raia wa kawaida, watashiriki, watashtakiwa kwenye Mahakama za kijeshi.
Hatua hii umezua mjadala mkubwa nchini Uganda, huku wanaharakati wa haki za binadamu, wakisema mpango huo wa serikali ni wa kushangaza.
Wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia, yameendelea kumshtumu kiongozi wa muda mrefu Yoweri Museveni, kutumia Mahakama za kijeshi kuwanyanyasa wapinzani wake.
Kuna hofu kuwa, iwapo mswada huo utapita, kesi inayomkabili kiongozi mkongwe wa upinzani Kizza Besigye ambaye amezuiliwa Gerezani kwa zaidi ya miezi mitano kwa madai ya kupanga kumdhuru rais Museveni na kushambulia vituo vya ulinzi, huenda ikarejeshwa kwenye Mahakama ya Kijeshi.