
Kufuatia uamuzi wa utawala wa Trump kusitisha misaada ya nje ya Marekani kwa siku 90, wizara ya afya ya Uganda imewapa wafanyakazi wa afya wanaofadhiliwa fursa ya kufanya kazi “kwa moyo wa kizalendo, kama watu wa kujitolea” wakati wa mazungumzo na Washington. Tangazo ambalo halikosi kuamsha hisia kwenye mitandao ya kijamii.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Ningeweza kulipa kodi yangu kwa uzalendo…?” “Huu ni aina ya ujumbe ambao umekuwa ukisambaa kwenye mtandao wa kijamii wa X nchini Uganda tangu serikali ilipoelekeza wazo katika siku za hivi karibuni kwamba wataalamu wa afya waliofadhiliwa hapo awali na misaada ya kimataifa kutoka Marekani wanaweza kufanya kazi kwa kujitolea.
Tangu Donald Trump alipoamua kusitisha msaada wa nchi yake nje ya nchi kwa siku 90, Wizara ya Afya ya Uganda, kwa mfano, imelazimika kufunga kliniki zote zilizobobea katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI na kuhamishia huduma za wagonjwa wao katika hospitali za umma. Uamuzi ambao bila shaka unabeba hatari ya msongamano wao, ndiyo maana mamlaka inaomba moyo wa uzalendo kwa wafanyakazi ambao sasa wamelazimika kubaki nyumbani, kwa lengo la kupunguza wimbi la wagonjwa hospitalini.
Kudumisha Pepfar, faraja ndogo sana
Wakati msamaha uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kwa “msaada muhimu wa kibinadamu” ambao Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) unamilikiwa – mojawapo ya programu kuu katika mapambano dhidi ya UKIMWI barani Afrika na mpango pekee nchini Uganda ambao haujaathiriwa na kusitishwa kwa misaada ya Marekani – unaonyesha faraja kidogo, hata hivyo hauondoi hali ya wasiwasi iliyokuwepo.
Wakati nchini Uganda, kiwango cha maambukizi ya VVU/UKIMWI kimeshuka kutoka 19% mwishoni mwa miaka ya 1990 hadi 5% mwaka 2024 na sasa inawahusu takriban watu milioni 1.5 tu, wataalamu wa afya katika sekta hiyo wana wasiwasi, kama kila mahali katika bara la Afrika, kuhusu athari za kiafya kwa kusitishwa kwa misaada ya kimataifa kutoka Marekani.