Mahakama Kuu nchini Uganda, imekataa kumpa dhamana mwanasiasa mkongwe wa upinzani Kizza Besigye na mshatakiwa mwenzake Hajji Obeid Lutale kwa madai kuwa wanakabiliwa na kesi ya uhaini, mashtaka ambayo uchunguzi wake bado unaendelea.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Uamuzi wa Jaji Kania ulisomwa na msajili wa mahakama kuu katika kitengo cha uhalifu Ssalaam Godfrey Ngobi.
Ssalaam Godfrey Ngoobi, msajili wa mahakama kuu kitengo cha uhalifu.
“Mashtaka dhidi ya washtakiwa ni kati ya yale makubwa kwenye vitabu vyetu vya sheria. Kutokana na ukweli kwamba upelelezi bado unaendelea, maslahi ya haki katika hatua hii yanaonyesha kuwa ombi la dhamana limekataliwa kwa sababu kuna uwezekano kwamba wakiachiliwa kwa dhamana wanaweza kuingilia upelelezi.”
Dkt Besigye na Hajji Lutale walitaka kuachiliwa kwa dhamana kwa madai kuwa upelelezi unachukua muda mrefu jambo ambalo linakiuka haki yao ya uhuru.

Wakili wao Erias Lukwago anasema kuwa uamuzi huo wa Jaji Kania ni wa kisiasa. Erias Lukwago Wakili wa Dkt Besigye na Hajji Lutale
“Huu ni uamuzi wa kutisha ambapo jaji amewahukumu kabla ya kusikiliza kesi! Inaathiriwa na mambo ya kisiasa na sio mambo ya sheria. Tutafanya mkutano na kuona hatua zilizopo ili kutafuta haki kutoka mamlaka nyingine inje ya Uganda kama vile mahakama ya Afrika Mashariki.”
Dkt Besigye na Lutale wamekuwa katika gereza la Luzira tangu tarehe 16 Novemba mwaka jana walipo kamatwa kutoka hoteli ya Riverside jijini Nairobi nakufungulia mashtaka ya kufanya njama ya kuipindua serikali ya Uganda kupitia mikutano kadhaa katika miji ya Geneva, Athens, Nairobi na Kampala.
Kenneth Lukwago, Kampala, RFI Kiswahili