
Ofisi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ilisema Jumanne kwamba maafisa 12 wa Algeria walifukuzwa kwa kulipiza kisasi baada ya Algeria kuamuru maafisa 12 wa Ufaransa kutoka wizara ya mambo ya ndani kuondoka nchini humo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Ofisi ya Rais wa Ufaransa hapo jana ilifahamisha kwamba rais Emmanuel Macron aliamua kuwatimua maafisa hao 12 wa ubalozi na kidiplomasia wa Algeria na kumrudisha nyumbani balozi wake kutoka Algiers, huku mzozo ukiongezeka kati ya nchi zote mbili.
Hatua hiyo ya kulipiza kisasi ilikuja baada ya koloni hilo la zamani la Ufaransa siku ya Jumapili kuamuru maafisa 12 wa Ufaransa kutoka wizara ya mambo ya ndani kuondoka ndani ya saa 48, kufuatia kukamatwa kwa afisa wake wa ubalozi jijini Paris kutokana na kuhusika na kukamatwa kwa mhamasishaji maarufu kwenye mtandao wa TikTok.
Ufaransa imeitaka Algiers kuanzisha tena mazungumzo, ikisema mamlaka ya Algeria imechukua jukumu la uharibifu wa ghafla wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.