Ufaransa: Nicolas Sarkozy ameachiliwa kwa masharti, bangili yake ya kielektroniki yaondolewa

Akiwa amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kufuatia kitendo chake cha kujaribu kumshawishi jaji katika kesi iliyokuwa inamkabili, Nicolas Sarkozy ameachiliwa kwa masharti, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Paris imetangaza Mei 15. Bangili yake ya kielektroniki imeondolewa baada ya miezi mitatu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya miezi mitatu chini ya uangalizi wa kielektroniki, mkuu huyo wa zamani wa nchi ya Ufaransa ameweza kufaidika na vifungu vya kisheria vilivyomuwezesha kuachiliwa kwa masharti. Kwa hiyo bangili yake ya kielektroniki iliondolewa Jumatano, Mei 14. Akiwa na umri wa miaka 70,  alikuwa ana haki ya kupata nafasi hiyo ya kuachiliwa kwa masharti, na kabla ya nusu ya kifungo chake.

Rufaa yake yakataliwa

Nicolas Sarkozy alihukumiwa mara ya kwanza Machi 1, 2021, kisha akakata rufaa Mei 17, 2023, na Mahakama ya Juu zaidi katika mfumo wa mahakama wa Ufaransa, ilikataa rufaa yake mnamo Desemba 2024. Kwa hiyo, rais huyo wa zamani wa Ufaransa alilazimika kutumikia kifungo chake.

Maendeleo

Hata hivyo, tangu Januari 28, siku yake ya kuadhimiha miaka 70 ya kuzaliwa kwake, alikuwa na uwezekano wa kuomba kupunguziwa kifungo, jambo ambalo hapo mwanzoni hakuonekana kulichagua, akielezea kwamba hakutaka “kutoa hisia ya kuomba nafasi hii.” Katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa X, alieleza kwamba anaachana na siasa, lakini aliendelea kudai kuwa ni mwathirika wa “ukosefu wa haki”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *