Ufaransa na Algeria zakubaliana kuanzisha upya mazungumzo ya kidiplomasia

Marais Wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Algeria Abdelamadjid Tebboune wamekubaliana kuanzisha upya mazungumzo yanayolenga kuimarisha mahusiano mapya ya kidiplomasia, kiuchumi, na usalama, baada ya miezi kadhaa ya mvutano baina ya nchi zao mbili.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ikulu ya rais champs Elysées jijini Paris Ufaransa, imefahamisha kuwa marais hao walizungumza kwa njia ya simu Jumatatu jioni, kujadili juu ya namna ya kuimarisha mahusiano mapya ya kidiplomasia, kiuchumi, na usalama, baada ya miezi kadhaa ya mvutano baina ya nchi zao mbili.

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune amesema ipo haja kwa nchi zao kutoendelea na mivutano ya kisiasa ambayo haisaidii maendeleo ya nchi zao, amesisitizia kile alichokisema kuanzisha tena ushirikiano zaidi kuhusu suala la uhamiaji lakini pia juu ya namna ya kukabiliana na ugaidi katika êneo la Afrika magharibi.

Mazungumzo ya viongozi hawa wawili yamefanyika baada ya ujumbe wa serikali ya Ufaransa kutembelea Algiers mara tatu ili kuweka misingi mipya ya uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Taarifa ya Ikulu ya Champs Elysee imesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noël Barrot na mwenzake wa sheriai, Gérald Darmanin, watafanya ziara ya kikazi siku ya jumapili ijayo jijini Algeirs Algeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *