
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema nchi yake itatumia Euro Bilioni 109 kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya Akili Mnemba, maarufu kwa jina la AI.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Tangazo hili la rais Macron linakuja wakati huu wadau mbalimbali wakikutana jijini Paris kuanzia siku ya Jumatatu, kwenye kongamano kubwa la kimatafa la siku mbili kujadili maendeleo ya Akili mnemba.
Ili kutangaza kongamano hilo kubwa, rais Macron amechapisha mikanda ya vídeo isiyokuwa halisi kuonesha uwezo wa teknolijia hiyo ambayo inashika kasi duniani, na kuibua maswali iwapo, itakuwa mbadala wa binadamu katika miaka inayokuja.
Mbali na Ufaransa, wawekezaji wengine ikiwemo nchi ya Falme za Kiarabu inatarajiwa kuwekeza pia kwenye miradi hiyo inayolenga kushindana na teknolojia kutoka Marekani ya Stargate, baada ya kuzindua mradi wa hadi Dola Bilioni 500 kuwekeza kwenye teknolojia ya ChatGPT.
Ufaransa, inatarajiwa kutumia kongamano hilo litakalohudhuriwa na wajumbe 1500 kutoka mataifa zaidi ya 100 kujadili fursa na changamoto za teknolojia ya Akili Mnemba katika dunia ya sasa.