
Maeneo mawili kati ya matano ya jeshi la Ufaransa nchini Senegal yatakabidhiwa rasmi kwa mamlaka ya Senegal leo Ijumaa, Machi 7, 2025. Hatua ya kwanza kuelekea uondoaji kamili wa wanajeshi wa Ufaransa nchini Senegal (EFS).
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff
Maeneo mawili ya kijeshi yanayoitwa maeneo ya Maréchal na Saint-Exupéry ambayo yanajumuisha kundi la nyumba na ghala zinazopakana na bustani ya Hann si mbali na bandari ya Dakar, kwa hiyo zinakabidhiwa rasmi mamlaka ya senegali.
Hakuna sherehe, lakini kusainiwa kwa ripoti kutaashiria uhamisho wa maeneo haya mawili kutoka kwa jeshi la Ufaransa kwenda jeshi la Senegal. “Taratibu rahisi,” kulingana na chanzo cha Senegal. Maeneo haya mawili yalikuwa hayana kitu kwa mwaka mmoja, kulingana na vyanzo vya jeshi la Ufaransa, yalikuwa yakingoja kukabidhiwa kwa Senegal.
Kisha kunasalia kurejeshwa kwa vituo vingine vitatu vya kijeshi vya Ufaransa, kimoja bandarini, kingine katikati mwa wilaya ya kati ya Ouakam na cha tatu, kituo cha wanajeshi wa kikosi cha majini kilicho kwenye lango la Dakar huko Rufisque. Ikiwa kupitishwa kwao chini ya bendera ya Senegal kutathibitishwa, mkutano wa pili wa tume ya pamoja ya Ufaransa na Senegali iliyoundwa kuandaa mipango ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa itaamua katika siku zijazo juu ya kasi ya makabidhiano yajayo.
Hatimaye, limesalia swali la Falcon 50, ndege ya jeshi la Ufaransa iliyoegeshwa kwenye uwanja wa ndege wa Dakar. Je, itasalia huko kuendelea kutekeleza kazi ya ufuatiliaji wa uvuvi na usafirishaji wa dawa za kulevya pamoja na mambo mengine kama Paris ingependa au itarejesha Ufaransa? Suala hilo bado halijaamuliwa, kulingana na vyanzo kadhaa.