Ufaransa kukabidhi kambi ya kijeshi ya Port-Bouët kwa jeshi la Côte d’Ivoire

Katika hafla ya sherehe ambapo Waziri wa Jeshi la Ufaransa, Sébastien Lecornu, na mwenzake wa Côte d’Ivoire, Téné Birahima Ouattara, watashiriki, Ufaransa itakabidhi rasmi kambi ya kijeshi ya Port-Bouët kwa jeshi la Côte d’Ivoire leo Alhamisi, Februari 20. Kambi hii hapo awali ilikuwa ikishikiliwa na kikosi cha 43 cha jeshi la wanamaji wa Ufaransa (BIMA).

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katika mji mkuu wa uchumi wa Côte d’Ivoire, bendera ya Ufaransa haitapepea tena juu ya kambi ya Port-Bouët, ambayo sasa itakuwa na jina la Jenerali Thomas-d’Aquin-Ouattara, kwa heshima kwa mkuu wa kwanza wa jeshi la Côte d’Ivoire. Baada ya Gabon majira ya kiangazi yaliyopita, Chad mwezi Januari, na kabla ya Senegal ambako Ufaransa bado ina wanajeshi 300, Paris itakabidhi rasmi kambi yake ya kijeshi iliyoko Abidjan kwa vikosi vya jeshi vya Côte d’Ivoire leo Alhamisi, Februari 20. Wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Jeshi la Ufaransa, Sébastien Lecornu, na mwenzake wa Côte d’Ivoire, Téné Birahima Ouattara, pia watatia saini mikataba mipya ya ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo, uhamisho wa majengo hayo kwa jeshi la Côte d’Ivoire – mchakato ulioanzishwa mwezi Aprili 2023 – ulianza wiki chache zilizopita, kwa lengo la kuruhusu kurekebisha kambi ya hekta 230 kulingana na mahitaji yake. Tangu Januari 20, kikosi cha askari wa miamvuli 90 wa Côte d’Ivoire wanaishi katika kambi hiyo, hasa wakithamini nafasi na ufikiaji wa miundombinuiliyowekwa sehemu hiyo. “Tuna uwezo wa kufikia miundombinu ambayo iko katika sehemu moja, ambayo inatuwezesha kutoa mafunzo kwa urahisi zaidi kuwa tayari kufanya kazi,” Kapteni Fabrice Yoboué Kouamé, mkuu wa kikosi cha askari wa miamvuli, amemwambia mwandishi wa RFI huko Abidjan, Bineta Diagne.

Wanajeshi wa Ufaransa wanatarajia kukamilisha kuondoka kwao ifikapo majira ya joto yajayo.