Ufaransa kuchunguza madai ya Haiti kuhusu kulipia uhuru wake

Tume ya pamoja ya wanahistoria wa Ufaransa na Haiti itachunguza suala lenye utata la kiasi cha pesa ambacho Paris ililazimisha koloni lake la zamani kulipia uhuru wake karne mbili zilizopita na kutoa mapendekezo, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amethibitisha.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ilitolewa jana na rais Emmanuel Macron na kuongeza kuwa mara tu kazi ya tume hiyo itakapokamilika, itawasilisha mapendekezo yake kwa serikali zote mbili.

Katika Kongamano la Kudumu la Umoja wa Mataifa la Watu Wenye Asili ya Afrika (PFPAD) la mwaka jana huko Geneva, muungano wa mashirika ya kiraia wa Haiti ulisema Ufaransa inapaswa kulipa mabilioni ya dola kama fidia kwa Haiti, baada ya kuilipa Ufaransa ili kupata uhuru wake.

Nchi hiyo ya Caribian ndio ya kwanza kupata uhuru wake mnamo 1804 baada ya uasi mkubwa wa uhuru wa watu waliokuwa watumwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *