Ufaransa: François Bayrou atishia kuvunja mikataba ya 1968 na Algeria

Waziri Mkuu François Bayrou alisema Jumatano tarehe 26 Februari kwamba hakuwa na nia ya kuingia katika “mzozo” na Algeria, lakini amebaini kwamba Ufaransa itaomba Algiers “kwamba mikataba yote” ya 1968 kati ya nchi hizo mbili ichunguzwe upya, la sivyohivyo “itavunjwa.” 

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

François Bayrou anasema Algeria inawajibika kwa shambulio la Jumamosi 22 Februari: “Waathiriwa tuliowaona huko Mulhouse ndio waathiriwa wa moja kwa moja wa kukataa kutekeleza makubaliano yake.” Janga linaloongeza orodha ndefu, kulingana na Waziri mkuu wa Ufaransa: “Kulikuwa na waathiriwa mwishoni mwa juma hili lililopita, kulikuwa na matukio mengine hapo awali. Kuna hali ya Boualem Sansal. Haya yote yanailazimisha serikali ya Ufaransa kutofumbia macho. “

Ufaransa “itaomba serikali ya Algeria kuangalia upya mikataba yote na jinsi (inavyotekelezwa),” alitangaza Waziri Mkuu wa Ufaransa, François Bayrou, siku ya Jumatano, akisema kwamba alikuwa akiipa Algiers makataa ya “mwezi mmoja, wiki sita.”

Akirejelea mikataba hii ya mwaka 1968 kati ya Ufaransa na Algeria, ambayo alisema “haikuheshimiwa”, François Bayrou alisema kuwa serikali ya Ufaransa haiwezi “kukubali hali iendelee”. “Wakati huo huo, orodha ya ‘dharura’ ya watu ambao lazima waweze kurejea nchini mwao na ambao tunawaona kuwa nyeti sana itawasilishwa kwa serikali ya Algeria,” aliongeza François Bayrou.

“Ikiwa hakuna jibu kwa hilo, hakuna shaka kwamba tutalazimika kuvunja makubaliano hayo na ndo njia muhimu inayowezekana,” mkuu wa serikali ya Ufaransa alionya, akihakikisha hata hivyo kwamba “hii sio njia tunataka.” “Ninasema haya bila nia yoyote ya kuongezeka kwa uhasam, bila nia yoyote ya mikataba hatarini”, lakini “ni jukumu la serikali ya Ufaransa kusema kwamba kukataa kwa raia wa Algeria ni shambulio la moja kwa moja kwa makubaliano ambayo tunayo na mamlaka ya Algeria na kwamba hatutakubali”.

François Bayrou pia alitangaza kwamba aliomba “ukaguzi wa mawaziri” kuhusu “sera ya utoaji wa visa” ya Ufaransa kutoka kwa wakaguzi wakuu wa polisi na Mambo ya Nje. Waziri Mkuu wa Ufaransa alikuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kamati ya wizara inayohusika na udhibiti wa wahamiaji (CICI) iliyokutana huko Matignon. Ombi la ukaguzi lilitiwa saini siku ya  Jumanne jioni kwa niaba ya ukaguzi mkuu wa polisi na maswala ya kigeni.

Moja ya hatua nyingine zilizochukuliwa baada ya mkutano huu wa kamati ya wizara inayohusika na udhibiti wa wahamiaji ni kuimarisha kijeshi mipaka ya nchi. “Matumizi ya nguvu ya mpaka, ambayo iliundwa na serikali ya Elisabeth Borne na kwa msingi wa majaribio, ilitumwa haswa kwenye mpaka na Italia. Kikosi hiki kitafanywa kwa ujumla kwa mipaka yote ya Ufaransa,” anaeleza François Bayrou. “Inaleta pamoja polisi, askari wa jeshi, forodha na inaturuhusu kuwaita askari wa akiba na jeshi la Sentinelle ikibidi ili mipaka yetu ifuatiliwe vyema. “

Mvutano unaongezeka kati ya nchi hizo mbili. Algiers imekataa mara kwa mara katika wiki za hivi karibuni kuruhusu raia wake kadhaa waliofukuzwa kutoka Ufaransa kuingia katika eneo lake. Uhusiano na Algiers, ambao tayari umedorora, umezorota zaidi kufuatia shambulio baya lililotekelezwa siku ya Jumamosi huko Mulhouse, mashariki mwa Ufaransa. Raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 37 katika hali isiyo ya kawaida anatuhumiwa kumdunga kisu mzee wa miaka 69 raia wa Ureno na kuwajeruhi watu wengine saba.