
Wakati AFC/M23, wakiungwa mkono na jeshi la Rwanda, wakiingia Bukavu mwishoni mwa juma hili , wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika walikuwa wakikutana mjini Addis Ababa kwa mkutano wao wa kila mwaka. Mzozo huo ulizusha majibizano makali siku ya Ijumaa jioni.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Kutoka kwa mwandishi wetu maalum mjini Addis Ababa,
Mwishoni mwa mkutano wa kilele siku ya Jumapili, hakukuwa na vikwazo wala kulaani waziwazi Rwanda kama ilivyotakiwa na DRC. Hakuna tangazo madhubuti juu ya mpango wa kumaliza mzozo. Vita hivi kati ya Rwanda na DRC vinaleta wasiwasi ndani ya Umoja wa Afrika, AU.
Ni nchi moja tu, Burundi, iliyoomba siku ya Jumapili, Februari 16, wakuu wa nchi kulaani Rwanda wakati wa kuhitimisha mkutano wao wa kilele. Lakini katika mkutano huo, “hakuna kiongozi hata mmoja aliyeweza kuunga mkono hoja ya Burundi,” amesema mshiriki mmoja. Katika mkutano huo, pia, wengi walikwepa suala hili la machafuko mashariki mwa DRC na wakachagua kulijadili kwa maneno yasiyoeleweka. Raila Odinga wa Kenya, alipoulizwa na mwandishi wa habari, alijibu tu: “Sitaki kuzungumzia suala hilo.”
Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama siku ya Ijumaa, uliojitolea kwa vita hivi, ulikuwa wa kusangaza. DRC ilitoa wito kwa AU kuiwekea vikwazo Rwanda kwa “uchokozi wake” dhidi ya eneo huru. Akiwa na hasira, Rais Kagame aliweka jukumu zima la mzozo huo kwa DRC. Mvutano ulikuwa mkubwa kiasi kwamba mkutano wa waandishi wa habari uliopangwa ulifutwa na saa 48 baadaye taarifa ya mwisho bado haijachapishwa.
Mchana, Kamishna wa Amani na Usalama, Bankolé Adeoyé, hata hivyo alifanya mkutano na waandishi wa habari na kutoa wito wa “kuondoka mara moja kwa M23 na wafuasi wake kutoka miji yote inayokaliwa.” Hakutaja Rwanda na pia alisisitiza juu ya haja ya “mazungumzo mapana na jumuishi ili kumaliza mgogoro huu.” Kwa upande wa Kongo, waridhika kwamba Kigali haikupata kiti ambacho nchi hiyo ilikuwa inatafuta ndani ya baraza hili la amani na usalama. “Kura ya kuiyadhibu”, kulingana na baadhi ya wachambuzi, hata kama mambo mengine yanaweza kuwa na jukumu na ushawishi wa Paul Kagame ndani ya AU unabaki kuwa muhimu sana.
Je, ni hatua gani zinazofuata za upatanishi?
“Vikwazo havijatatua matatizo kila mara,” alisema Rais wa Kongo-Brazzaville, Denis Sassou Nguesso, kwenye kituo cha France 24 siku ya Jumapili “Kilicho muhimu kwetu ni kutafuta suluhu la kweli la mgogoro.”
Katika suala hili, wakuu wa nchi waliidhinisha kimsingi kuunganishwa kwa michakato miwili ya Luanda na Nairobi ili kuepusha kuingiliwa kati ya njia tofauti za upatanishi, lakini hakukuwa na ufafanuzi juu ya utekelezaji wa muunganisho huu.
Miongoni mwa maswali yanayoibuka: lile la mustakabali wa wapatanishi wa sasa, Mkenya Uhuru Kenyatta, na Joao Lourenço wa Angola, ambaye sasa anashikilia urais wa zamu wa Umoja wa Afrika, AU, na ambaye rais wa Rwanda anamchukulia kuwa karibu sana na misimamo ya Kinshasa.