Uchumi wa Ujerumani kukuwa kwa miaka miwili mfululizo

Haya ni kulingana na taasisi ya kiuchumi ya Ifo inayotarajia kuwa hatua mpya zinazochukuliwa na serikali na ongezeko la matumizi kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi hiyo ambao kwa sasa hauko katika hali nzuri.

Ifo inasema inatarajia uchumi wa Ujerumani ukuwe kwa asilimia 0.3 mwaka 2024, kinyume na ilivyokuwa imetabiriwa awali kwamba utakuwa kwa asilimia 0.2.

Kwa mwaka 2026, taasisi hiyo ya kiuchumi inatarajia uchumi wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi Ulaya, kukuwa kwa asilimia 1.5 kinyume na ilivyokuwa imebashiri awali kwamba ungekuwa kwa asilimia 0.8.

Kansela wa Ujerumani (kulia) akiwa na viongozi wengine wa serikali katika bunge la Ujerumani, Bundestag
Kansela wa Ujerumani (kulia) akiwa na viongozi wengine wa serikali katika bunge la Ujerumani, BundestagPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

“Mgogoro wa uchumi wa Ujerumani ulifikia hatua yake mbaya zaidi kabisa katika nusu ya mwaka ya majira ya baridi,” alisema Timo Wollmerhaeuser, mkuu wa taasisi ya Ifo. “Sababu moja ya kukuwa huku ni hatua za kifedha zilizotangazwa na serikali mpya.”

Wiki iliyopita baraza la mawaziri la Ujerumani liliidhinisha kitita cha yuro bilioni 46 kama fedha za kupunguza mzigo wa kodi kwa makampuni, na kuufufua uchumi wake unaokuwa kwa kasi ndogo kuanzai mwaka 2024 hadi 2029.

Bunge la Ujerumani pia mnamo mwezi Machi, liliidhinisha mipango ya kuongeza pakubwa matumizi ikiwemo yuro bilioni 500 za kuimarisha miundo mbinu na kuondoa pakubwa uwekezaji katika ulinzi kutoka kwenye sheria zinazotilia kikomo kuchukua mikopo.

Katika ubashiri wake wa kiuchumi, taasisi ya Ifo inakadiria ongezeko la yuro bilioni 10 mwaka 2025 na yuro bilioni 57 mwaka 2026 kutokana na hatua hizo zilizochukuliwa na serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *