
Waziri Mkuu wa Jahuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) Judith Suminwa amezindua siku ya Jumamosi, Machi 1, kampeni ya kitaifa ijulikanayo kwa Lingala kwa jina la: “Congolais Telema ” (ikitafsiriwa kwa Kiswahili: Wakongo simammeni) kulinda nchi dhidi ya uvamizi wa Rwanda.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Kampeni hiyo imezinduliwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa, RTNC mjini Kinshasa.
Kulingana na Radio OKAPI, Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa kampeni hii ni sehemu ya vita vya kiraia ambavyo DRC inaongoza kando ya nyanja ya: kijeshi, kidiplomasia, vyombo vya habari, mahakama na kiuchumi ili kuwafukuza wavamizi nje ya nchi. Judith Suminwa pia ameeleza kuwa kupitia mpango huu, Wakongo wanawajibika kutetea ardhi yao, popote walipo: ndani na nje ya nchi.
Kampeni hii imezinduliwa mbele ya baadhi ya wajumbe wa Serikali na watu kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wanafunzi na wanamichezo wa nchi hiyo.