
Siku ya Jumatano, Juni 11, Tume ya Uchaguzi ya Burundi imetangaza matokeo ya muda ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika Juni 5. Wakati CNDD-FDD, chama tawala, kikiibuka mshindi wa wazi kwa zaidi ya asilimia 96 ya kura, wapinzani wake wameshutumu udanganyifu wa wazi na kusema kuwa uchaguzi huo kuwa “uliibiwa.”
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku sita baada ya uchaguzi uliopingwa wa Juni 5 ambapo Warundi walichagua wabunge wao na madiwani wa manispaa, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) imetangaza matokeo ya muda ya uchaguzi huo wa wabunge wakati wa sherehe rasmi mjini Bujumbura Jumatano, Juni 11.
CNDD-FDD, chama ambacho kimeitawala Burundi kwa mkono wa chuma tangu mwaka 2005, ndicho kimeibuka mshindi kwa zaidi ya 96% ya kura zilizopigwa. Vyama vingine 20 vya kisiasa na miungano iliyoingia kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi, hata hivyo, wanasema uchaguzi huo uliibiwa, na hakuna aliyepata zaidi ya 1% ya kura, isipokuwa chama cha zamani cha Uprona, kilichoshika nafasi ya pili kwa 1.3% ya kura. Kutokana na matokeo haya, katibu mkuu wake, Olivier Nkurunziza, mara moja alichukua nafasi ya kuyapinga, na kuyataja kuwa ya “ushabiki” na kushtumu uchaguzi “ulioibiwa”.
“Matokeo haya yanaonyesha kukataa kwa chama tawala kukubali demokrasia” , amesma Olivier Nkurunziza, Katibu Mkuu wa UPRONA
Kwa vyovyote vile, matokeo haya yanaruhusu chama cha rais Évariste Ndayishimiye kushinda viti vyote 100 katika Bunge la taifa. Kulingana na Katiba ya Burundi, ni vyama vinavyopata zaidi ya 2% ya kura pekee ndivyo vinavyostahiki kujiunga na Bunge la taifa. Hata hivyo, Bunge jipya litakuwa na jumla ya wabunge 111 katika kipindi hiki, huku wawakilishi wanane wa kuchaguliwa kutoka jamii ya Wahutu na watatu kutoka jamii ya Twa wakishirikiana kuakisi uwiano wa kikabila nchini humo—60% ya Wahutu, 40% ya Watutsi na 3% ya Twa—kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Msingi.
Mapema Juni 5, vyama vingi vilivyoshiriki katika uchaguzi vimeshutumu uchaguzi uliogubikwa na “makosa makubwa” na nia ya kuanzisha “chama kimoja” nchini Burundi. Ingawa CENI inadai kuwa kuna uwezekano wa kuwasilisha rufaa kwa Mahakama ya Kikatiba kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho Juni 24, matokeo yao “hayana matumaini yoyote,” kulingana na wapinzani kadhaa.