
Chama tawala cha CNDD-FDD cha Rais Evariste Ndayishimiye kinatuhumiwa kwa kuhujumu mpinzani wake mkuu, National Freedom Council – CNL, ambacho kilimaliza katika nafasi ya pili kwenye uchaguzi uliopita wa 2020 na kikadai kuwa matokeo yalichakachuliwa.
Mnamo mwaka wa 2023, wizara ya mambo ya ndani ilikifungia chama cha CNL kuhusiana na kile ilichokiita “makosa” katika namna kilivyoandaa mikutano yake.
Kisha mwaka jana, CNL kilimfukuza kiongozi wake, kamanda wa zamani wa wanamgambo aliyegeuka kuwa mwanasiasa Agathon Rwasa, wakati alipokuwa nje ya nchi. Nafasi yake ilichukuliwa na mtu anayefikiriwa kuwa karibu na chama tawala, Nestor Girukwishaka, waziri wa zamani na mtendaji mkuu katika kampuni inayomilikiwa na serikali — katika kile wakosoaji walichoeleza kama mapinduzi yaliyopangwa na serikali. Kisha serikali ilipitisha sheria mpya ambazo zilimzuia Rwasa na washirika wake kujiunga na vyama vingine vya upinzani au kushiriki katika uchaguzi kama wagombea wa kujitegemea.