Ubelgiji yalilaumu vikali Baraza la Usalama kwa kushindwa kulinda misingi ya Hati ya UN

Naibu waziri mkuu wa Ubelgiji Maxime Prevot amesema “amesikitishwa sana” kuona Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kutuma ujumbe wazi wa kuunga mkono sheria za kimataifa, na akatoa wito wa kuchukuliwa hatua kali zaidi za kimataifa za kulinda haki za binadamu na kuwawajibisha wakiukaji wa sheria.