Uamuzi wa ICC wa kutiwa mbaroni Netanyahu na mshirika waendelea kupongezwa

Mataifa na shakhsia mbalinmbali ulimwenguni wameendelea kupongeza uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wa kutoa hati ya kukamatwa Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na aliyekuwa waziri wake wa vita Yoav Gallant, wakituhumiwa kutenda jinai za vita.

China imeitaka mahakama ya ICC kuwa na utendaji wa haki katika maamuzi yake na kukosoa undumakuwili wa baadhi ya mataifa ya dunia kuhusiana na uhalifu na jinai za kivita.

Lin Jian, msemaji katika Wizara ya mambo ya kigeni ya China, ameishutumu Marekani kwa kutokuwa na msimamo kuhusu suala la ICC, ambapo inapinga kukamatwa kwa Benjamin Netanyahu, lakini uunga mkono kukamatwa kwa rais  wa Russia Vladimir Putin.

Stéphane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaheshimu utendaji na mamlaka ya mahakama hiyo.

Josep Borrell Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema: Amri ya Mahakama ICC dhidi ya Netanyahu na Gallant sio ya kisiasa na uamuzi huo lazima uheshimiwe na kutekelezwa.

Uswisi, Uholanzi na Ubelgiji sambamba na kupongeza uamuzi huo zimetangaza kuwa, zitamtia mbaroni Netanyahu endapo atakwenda katika mataifa hayo.

Waziri Mkuu wa Canada na Waziri wa Ulinzi wa Italia wamesifu uamuzi huo na kueleza kwamba, hiyo ni hatua ambayo wao walikuwa wakiitaka tangu awali.

Rais waa Combia amesema kuwa, Netanyahu ametenda jinai za kivita na mahakama ya ICC imethibitisha hilo hivyo ni lazima kuheshhimu uamuzi huo.