TZ Green yaanza kibabe TCA Majaribio

BAADA ya kupoteza mara nyingi dhidi ya TZ Blue katika mechi za majaribio kwa ajili ya kusaka kikosi cha timu ya taifa ya kriketi, TZ Green, hatimaye imeweza kufuta uteja baada ya ushindi wa mikimbio 32 kati mechi ya kwanza katika Uwanja wa UDSM mwishoni mwa juma.

Wachezaji nyota  wa kriketi wamejigawa katika timu za TZ Green na TZ Blue na watakuwa wakicheza mechi za mara kwa mara ili kuiwezesha Tanzania kuwa na kikosi imara cha timu ya taifa kwa ajili michuano mikubwa ya kimataifa, kwa mujibu wa msemaji wa chama cha kriketi nchini (TCA), Ateef Salim.

Mechi hii ya kwanza ya kusaka kikosi, ilishuhudiwa vijana wa TZ Green wakianza kubeti na kutengeneza mlima wa mikimbio 170 huku wakipoteza wiketi 6 baada ya kumaliza mizunguko yote 20 ya mchezo.

Mambo yalikuwa mazito kwa TZ Blue katika azma yao kufukuzia alama za wapinzani wao baada ya jitihada zao kugota kwenye mikimbio 138 baada ya kutumia mizunguko 19 kati ya 20 ya mchezo huo na hivyo kujikuta wakipoteza kwa mikimbio 32.

Aliyewaua TZ Blue ni Umar Shaikh ambaye peke alichangia mikimbio 65 kutokana na mipira 46 na alisaidiwa sana na mkongwe Kassimu Nassoro ambaye alichangia mikimbio 58 kutokana na mipira 33 bila kutolewa.

Ingawa hawakiweza kuisadia timu ya TZ Green kupata ushindi, lakini Abdulrazak Mohamed Amiri aliyepiga mikimbio 43, Raymond Francis aliyepiga mikimbio 42 na kushinda wiketi 2, na mkongwe Ally Mpeka aliyepiga mikimbio 30, walikuwa na mchezo mzuri katika mechi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *