
TWIGA Stars inatarajiwa kushuka uwanjani jioni ya leo kuisaka tiketi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 itakapovaana na Guinea ya Ikweta, ambapo kocha mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime amesema kikosi hicho kimekamilika kwa asilimia 80.
Fainali zijazo za WAFCON 2026 zitafanyika Morocco na leo Twiga itashuka kwenye Uwanja wa Azam Complex kabla ya kurudiana Februari 26 ambapo atakayependa hapo atakutana na mshindi kati ya Uganda na Ethiopia kwenye raundi ya pili.
Shime amesema kwamba asilimia 80 ya wachezaji wake wako tayari kwa ajili ya mchezo huo muhimu na wengine walitarajiwa kuwasili kambini jana.
“Ni mchezo muhimu sana kila mchezaji anafahamu, baadhi ya wachezaji wanaocheza nje ya Afrika walichelewa lakini waliopo wanajua nini cha kufanya kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu,” amesema Shime na kuongeza:
“Kuchelewa kwao kunaweza kuathiri kwa kiasi fulani ila tuliokuwa nao wanafahamu falsafa yetu na ni mchezo muhimu sana wa kutupatia nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia, tutangalia afya zao wakirejea wakowa sawa tunaweza kuwatumia kwa muada gani.”
Hadi sasa Opah Clement, Julietha Singano (FC Juarez ya Mexico), Enekia Lunyamila (FC Mazaltan), Aisha Masaka wa Brihton na Malaika Meena wa Bristol City ya Uingereza ndio nyota ambao wako njiani wakichelewa kujiunga na kambi.
Kwa upande wa Kocha wa Guinea, Guillermo Ganet amesema wanafahamu ubora wa nyota wa Tanzania lakini kama kocha ameandaa kikosi chake kwa ajili ya kupata pointi tatu.
“Tanzania imeendelea kwenye soka la wanawake, tunajua tunakutana na wapinzania wa aina gani naamini utakuwa mchezo mgumu na mzuri lakini kwetu tutapambana kupata pointi tatu.”
GUINEA HAWAJAPOA
Sio mchezo rahisi kwa Twiga kutokana na ubora wa wapinzani wao kwenye mashindano ya kimatifa hadi viwango vya CAF ikiwa nafasi ya pili kwa timu zilizoweka rekodi.
Timu hiyo imeshachukua ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wanawake mwaka 2008 ikiitandika Afrika Kusini mabao 2-1 wakati ambao wakati ambao Guinea ndio walikuwa wenyeji wa mashindano hayo.
Mwaka 2010 ikashiriki tena na kumaliza nafasi ya pili baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-2 na Nigeria, kisha 2012 ikabeba ndoo ikiitandika tena Banyana Banyana mabao 4-0.
Ukitazama ni wapinzani ambao Tanzania inapaswa kuwa makini nao hasa kwenye hatua hizi za mtoano ambazo timu hiyo inapambana kuhakikisha inashiriki Kombe la Dunia.
HAWA HATARI
1.Dorine Chuigoue
Huyu ndio nahodha wa timu ya Guinea mwenye umri kubwa akiwa na miaka 36 na mafanikio makubwa kimataifa ambaye kwa sasa akikipiga Real Betis ya Hispania.
Ni beki wa kati mwenye nguvu wa uwezo wa kuwakaba washambuliaji ameshacheza Dux Lugrono ya Hispania ambaye pia aliwahi kuichezea Clara Luvanga anayezima Al Nassr ya Saudia.
Ana uzoefu mkubwa kwani tayari ameshacheza mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2011 akiitafuta rekodi nyingine, mbali na kukaba ni mzuri kwenye mipira ya kona na mbali na huyu anapaswa kuangaliwa zaidi.
2.Diana Meriva
Ni winga kinda kwenye timu hiyo akiwa na miaka 22, nyota huyo anakipiga Famalicao ya Ureno na amecheza WAFCON ya mwaka 2018.