
Nchini Tunisia, kesi ya madai ya kula njama dhidi ya usalama wa taifa inatarajiwa kufunguliwa leo Jumanne, Machi 4. Inahusu takriban watu arobaini, wakiwemo viongozi saba wa kisiasa, ambao wamefungwa jela kwa miaka miwili.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Kesi hii itafunguliwa leo Jumanne, Machi 4 nchini Tunisia. Wakishutumiwa kwa “njama dhidi ya usalama wa taifa,” wapinzani kadhaa wa Rais Kaïs Saïed watafikishwa mbele ya mahakama mjini Tunis. Viongozi wa chama, wanasheria, viongozi wa vyombo vya habari: karibu watu arobaini kutoka makundi mbalimbali wanafunguliwa mashitaka.
“Kesi iliyotengenezwa na mahakama”, kulingana na mmoja wa wafungwa
“Raia wa Tunisia watagundua ukweli kuhusu mbin hii potovu ya mahakama. Watajua ni nani aliyesaliti, aliyepanga njama, nani alidanganya na wahalifu wa kweli ni akina nani.” Maneno haya yaliandikwa na wakili Jaouhar Ben Mbarek, mmoja wa wafungwa katika kesi ya kula njama, siku chache kabla ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza, katika barua iliyotumwa kwa Watunisia. Atafikishwa mbele ya jaji leo Jumanne kupitia kupitia njia ya video na wafungwa wenzake.
Khayem Turki, mwanasiasa, Abdlehamid Jelassi, mwanachama wa chama cha Kiislam cha Ennahda, Ghazi Chaouachi, mbunge wa zamani na katibu mkuu wa chama cha mrengo wa kushoto cha Democratic Current, Issam Chebbi, kiongozi wa chama cha Al Joumhouri, Ridha Belhaj, wakili na mwanachama wa chama cha Nidaa Tounes, wanashutumiwa kwa kula njama kwa msaada wa mfanyabiashara maarufu nchini Tunisia, Kamel Kamel. Washtakiwa wengine wawili, mwanaharakati Chaima Issa na wakili Lazar Akremi, watafikishwa mahakamani wakiwa huru.
Njama hii inayodaiwa, ambayo maelezo yake hayajulikani sana, inatokana na ushuhuda wa watu watatu wasiojulikana pamoja na majibizano ya kutiliwa shaka kati ya washtakiwa na makansela wa kigeni. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameitisha maandamano nje ya mahakama.
Tunatuhumiwa kuwa wananadharia wa njama, wasaliti, wahusika wa maovu yote ambayo Tunisia inapitia, anasema wakili Brahim Belghith, mwanasheria huko Tunis, ambaye anashutumu “ukiukwaji mkubwa wa haki za kesi ya haki”
RFI
Familia na mawakili wanahofia kusikilizwa kwa kesi ya mfano kwa upinzani kwa Rais Kaïs Saïed, huku mamlaka ikihakikisha uhuru wa haki nchini humo na masharti ya kusikilizwa kwa haki.
Vita vya vyombo vya habari
Kwa wiki moja sasa, kesi ya njama dhidi ya usalama wa taifa imekuwa mada ya vita vya vyombo vya habari, ambayo inaonyesha mvutano unaozunguka jambo hili. Baada ya vyombo vya habari kuingilia kati na kampeni kwenye mitandao ya kijamii na mawakili wa washtakiwa ambao walishutumu kesi “tupu”, wanaojiita watetezi wa serikaliwako tayari kwa jambo lolote kutokea.
Siku ya Ijumaa jioni, Riadh Jrad, mwandishi wa safu zenye utata, alizungumza kwenye televisheni ya kibinafsi baada ya kutangazwa kwa ripoti kuu juu ya madai ya njama hiyo. Aliweka maelezo ya kesi hiyo na nyaraka ambazo uaminifu wake unabaki kuthibitishwa. Kutangazwa kwa kipindi hicho kulizua wimbi la hisia ndani ya upinzani, ambao ulishutumu upendeleo kwa serikali na propaganda za kuwadhalilisha wafungwa katika suala hili.
Kwa sasa, mahakama imetangaza kuwa kesi hiyo itasikilizwa kwa njia ya video, ikimaanisha kuwa wafungwa hao hawatakuwepo mahakamani na wataonekana kwa njia ya video kwa sababu za kiusalama.