‘Tunampoteza mtu bora zaidi kati yetu’: Waajentina waomboleza kifo cha ‘Papa wao’ Francis

Katika nchi ya asili ya Francis, hisia zimekuwa zikipandaongezeka tangu kutangazwa kwa kifo cha kiongozi wa kanisa Katoliki dunia Papa Francis mnamo Aprili 21, na umati wa watu kumkumbuka papa unaandaliwa katika mji mkuu wa Argentina.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Buenos Aires, Théo Conscience

Mbele ya Kanisa Kuu la Buenos Aires, umati wa waumuni umekusanyika kuomboleza kifo cha mpendwa wao Papa Francis chini ya mvua kubwa. Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu saa 8:30 asubuhi (saa za Argentinahuko) kwa ajili ya kumuenzi Papa Francis. “Sifa nzuri zaidi ambayo sisi Waajentina tunaweza kumkumbukia Francis ni kuungana.” Askofu Mkuu wa Buenos Aires, Jorge García Cuerva, anatoa mahubiri ya kifo cha Papa Francis, Jorge Mario Bergoglio,” inasomeka chapisho hilo kwenye televisheni ya umma ya Argentina, ambayo imerusha video ya misa kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Licha ya kumalizika kwa misa hiyo, watu waliendelea kufika na kutoa heshima zao. Watu wengi walioamshwa kwa taarifa za kifo cha Francis waliona haja ya kuja kutoa heshima zao kabla ya kwenda kazini.

Papa Francis, “Muargentina muhimu zaidi katika historia”

Papa wa kwanza wa Amerika ya Kusini na papa wa kwanza wa Argentina katika historia, Francis pia alikuwa chanzo cha fahari na msukumo kwa wenzake wengi, kama Diego, mwanafunzi wa miaka 27. “Kwangu mimi, yeye ndiye Muajentina muhimu zaidi katika historia, kwa kila kitu alichofanikisha na kile anachowakilisha. Na kwa kufanikiwa kufufua nchini Argentina huruma na unyenyekevu ambao umetuonyesha kwa muda mrefu na ambao tumepoteza katika siku za hivi karibuni,” anasema Diego.

“Leo si tu kumpoteza papa, tunapoteza aliye bora zaidi kati yetu,” amesema kijana mmoja ambaye alichagua kutokwenda darasani. Maneno yanayorudi kwenye vinywa vya Waajentina wengine.

Waajentina wamepoteza mmoja wao, ambaye wangeweza kutambua. Mtu rahisi, anayeweza kufikiwa, shabiki wa kandanda pia, kwani Papa alikuwa shabiki wa kilabu cha San Lorenzo, katika mtaa wake wa asili wa Flores huko Buenos Aires, ambapo sherehe zingine zimepangwa leo na katika siku zijazo.

Licha ya kutofautiana kwake na Papa Francis, Rais wa Argentina Javier Milei amekiri umuhimu aliokuwa nao kwa wananchi wake kwa kutangaza maombolezo ya kitaifa ya siku saba.

“Licha ya tofauti zinazoonekana kuwa ndogo leo, kuweza kumjua kwa wema na hekima yake ilikuwa heshima ya kweli kwangu,” rais wa Argentina ameandika kwenye chapisho kwenye ukurasa wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *