Tuna taarifa Rwanda inapanga kutuvamia: Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye

Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye ameliambia shirika la habari la Uingereza BBC kwamba amepata taarifa za kijasusi za kuaminika kwamba Rwanda inapanga njama ya kuivamia nchi yake.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Ndayishimiye pia ameeleza kwamba nchi ya Rwanda ilijaribu kutekeleza mapinduzi ya kijeshi nchini Burundi mwongo mmoja uliopita, jambo ambalo amelifananisha na kinachofanyika DRC kwa sasa.

Rwanda tayari imejibu kauli za rais wa Burundi ikizitaja kama za kushangaza na kwamba nchi hizo mbili jirani zinashirikiana katika mipango ya kiusalama katika eneo la mpaka yao ambao hata hivyo umesalia kufungwa kwa zaidi ya mwaka moja sasa.

Rwanda imendelea kukanusha madai ya kuhusishwa na kuibukia upya kwa kundi la waasi wa Red Tabara, kundi ambalo rais Ndayishimiye anasema lina agenda sawa na lile na M23 ambalo linaelezwa kupata usaidizi kutoka kwa Rwanda.

Rais wa Burundi anasema Rwanda inawatumia waasi wa Red Tabara kuiyumbisha nchi yake kama namna inavyofanya nchini DRC kwa kuwatumia waasi wa M23.
Rais wa Burundi anasema Rwanda inawatumia waasi wa Red Tabara kuiyumbisha nchi yake kama namna inavyofanya nchini DRC kwa kuwatumia waasi wa M23. REUTERS – Arlette Bashizi

Ndayishimiye anasema Rwanda inataka kulitumia kundi hilo na waasi wa Red Tabara kuiyumbisha Burundi.

Licha ya ushahidi kutoka kwa Umoja wa Mataifa na nchi ya Magharibi kwamba Rwanda inawaunga mkono waasi wa M23 pamoja na kupigana pamoja nao mashariki ya DRC, Kigali imeendelea kukanusha ripoti hizo.

Tangu waasi wa M23 wanaosaidiwa na wanajeshi wa Rwanda kuanza kuteka maeneo mbalimbali mashariki ya DRC mwezi Januari, mamilioni ya watu wamelazimika kupoteza makazi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *